BENDERA ZA CATALUNYA ZAIPONZA BARCELONA, YAPIGWA FAINI YA SH MILIONI 345
Shirikisho
la Soka Ulaya (Uefa) limeipiga faini Barcelona kwa kutumia bender za
kisiasa katika moja ya mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Barcelona imetwanga faini ya euro 150,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 345.
Mashabiki
wa Barcelona walitumia bendera maarufu za Estelada ambazo ni maarufu
kwa wale mashabiki wa siasa wanaotaka sehemu ya Catalunya kujitenga na
Hispania.
Uefa imesema suala hilo ni la kisiasa na Barcelona wanajua suala hilo si sahihi. Hata hivyo wamepewa nafasi ya kukata rufaa.
Hivi karibuni, Barcelona ilipewa onyo wakati wa fainali ya Copa del Rey kuhakikisha hakuna matumizi ya bendera hizo.
Post a Comment