SERENGETI BOYS WAPATA SARE NYINGINE DHIDI YA MALAYSIA KATIKA MICHUANO YA INDIA
Timu
ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys wamepata sare
nyingine baada ya Malaysia kusawazisha mabao yote mawili waliyotangulia
kufunga vijana hao.
Mechi hiyo ni ya michuano ya Kombe la Vijana la AIFF inayofanyika katika mji wa Goa nchini India.
Boys
walianza kupata bao lao la kwanza katika dakika ya 31 kupitia
mshambuliaji wao hatari, Asad Ali Juma na Yohana Oscar akaongeza la pili
katika dakika ya 59, ikiwa ni dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi
cha pili.
Makosa ya walinzi, yaliwaruhusu Malaysia kusawazisha mabao yote mawili ndani ya dakika tano tu.
Walianza kupata bao la kwanza katika dakika ya 63 kupitia Arif Suhaimi na Najmi Idhar akafunga la pili katika dakika ya 68.
Hii
ni sare ya tatu kwa Boys zikiwemo zile za 1-1 dhidi ya Marekani, 2-2
dhidi ya Korea na imepata ushindi mmoja wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji
India. Inaendelea kuwa haijapoteza hata mechi moja katika michuano hiyo.
Post a Comment