Ne-Yo Ametua Bongo Tayari Kwa Kutoa Burudani Tamasha La Jembeka
Mwanamuziki
mahiri kutoka nchini Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu kwa jina
la NE-YO amewasili jana usiku katika uwanja wa ndege wa kimtaifa wa
Julius Nyerere (JNIA) tayari kwa kutoa burudani ya aina yake katika
tamasha kubwa la “Jembeka Festival” litakalofanyika kesho tarehe 21 May
jijini Mwanza. Mara baada ya kuwasili msanii huyo alisema alipelekwa
katika hotel ya Hyatt Regency ambako yeye na timu yake nzima wamefikia
na baadaye alijumuika na waalikwa wachache katika “Meet & Greet
Party”
Akizungumza mara baada ya NE-YO kuwasili
hotelini hapo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao
alisema “tumefurahi sana kuwa na NE-YO hapa Tanzania na tunataka
kuhakikisha kwamba tunawapatia wateja wetu burudani ya Tamasha la
Jembeka Festival 2016 limeandaliwa na kampuni ya Jembe chini ya udhamini
mkuu wa kampuni ya mawasiliano nchini Vodacom Tanzania litafanyika
katika uwanja wa CCM Kirumba. Vodacom Tanzania imedhamini ujio wa
mwanamuziki huyu ili kuwapatia burudani ya kimataifa wateja wake na
watanzania wote kwa ujumla. NE-YO ambaye ataimba steji moja na
wanamuziki wa Tanzania wakiwemo Fid Q, Juma Nature, Mr Blue na wengine
wengi, sambamba nao pia atakuwepo mwanamuziki nyota wa Afrika Mashariki,
Diamond Platnumz. Kumbuka wawili hawa wako katika matayarisho ya ngoma
yao ambapo Diamond amemshirikisha NE-YO na kwa mujibu wa Diamond
Platnumz watatambulisha wimbo huo hapo kesho katika tamasha la “Jembeka
Festival”
Mkurugenzi
wa Vodacom pia aliwahimiza wapenda burudani wote kununua tiketi zao
mapema kujiandaa na tamasha kubwa la aina yake hapo kesho. Wateja wa
Vodacom wanaweza kununua tiketi kuhudhuria tamasha hili kubwa kupitia
M-Pesa kwa kufuata hatua zifuatazo.
1. Piga *150*00# chagua 4 LIPA KWA M-PESA
2. Chagua 3 CHAGUA KWENYE ORODHA
3. Chagua 2 MANUNUZI
4. Chagua 3 JEMBEKA FESTIVAL
5. Weka namba ya kumbukumbu – 200200
6. Weka kiasi
7. Weka PIN yako ya M-PESA
8. Bonyesha 1 kuthibitisha.
Tukutane Jembeka Festival
Unaweza kufahamu zaidi kuhusu mtandao wa 4G na maeneo unapopatikana kwa kubofya HAPA
Post a Comment