HATIMAYE UCHAGUZI YANGA WASOGEZWA MBELE, SASA UTAKUWA JUNI 25
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), limetangaza kusogeza mbele uchaguzi mkuu wa
Yanga uliokuwa umepangwa kufanyika Juni 5, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya TFF, Aloyce Komba, amesema uchaguzi huo umesogezwa mbele hadi Juni 25, mwaka huu.
Awali,
Yanga ililalamika ikidai uchaguzi huo usogezwe ili wapate nafasi ya
kufikiria zaidi mashindano yaliyo mbele yao ambayo ni ubingwa wa Ligi
Kuu Bara wanaouwania, fainali ya Kombe la FA na michuano ya Kombe la
Shirikisho. Hata hivyo, mwanzoni TFF iliweka ngumu kuhusiana na madai ya
Yanga.
“Tumeyafanyia
kazi maombi ya Yanga na kamati ilikutana, tukajadiliana na kuamua
kusogeza mbele ili kuipa nafasi Yanga kwenye mashindano ya ligi kuu,
fainali ya Kombe la FA na Kombe la Shirikisho.
“Wakati
wanajiandaa kumalizia ligi pia wawe wanajiandaa kwa ajili ya uchaguzi
ili visiwepo tena visingizio vingine mbeleni. Muda tuliowapa unawatosha
kabisa,” alisema Aloyce.
Hata
hivyo, tamko la Aloyce linapingana na kauli aliyowahi kuisema kuwa
hawatabadilisha chochote kuhusiana na uchaguzi, hali ambayo inaonyesha
wamezidiwa nguvu na hoja za Yanga.
Post a Comment