Diamond Dharau 100%, amekuwa na dharau tokea akaunti yake benki isome shilingi bilioni 8
Madai! Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenyooshewa kidole na baadhi ya watu wake wa karibu tangu kitambo wakidai kuwa, toka kuukwaa umaarufu kupitia sanaa hiyo na kusemekana akaunti yake benki inasoma shilingi bilioni 8, amekuwa na dharau wakiitaja ni kwa asilimia mia moja, Amani lina kila kitu.
Kwa mujibu wa watu hao, wakiwemo
waliyosoma naye shule ya sekondari, Diamond wa sasa si yule wa zamani
kwa vile ana fedha nyingi na ana jina kubwa huku pia akijulikana
kimataifa.
“Jamani nataka kuwaambia jambo moja
kuhusu dogo Diamond. Huyu jamaa tangu amepata jina na tangu amekuwa na
akiba benki sijui bilioni nane, hashikiki. Maana nilisoma kwenye
mtandao, basi anajisikia sana.
“Imefika mahali dogo nampigia simu
hapokei wala nikimtumia meseji hajibu. Hii mimi naona ni dharau kwa
asilimia mia moja. Diamond amesahau nyuma alikotoka. Mimi sasa ni kama
shabiki wake, kwa hiyo asisahau kwamba ndiyo tumemfikisha alipo.”
KUMBE WAPO WENGI
“Na hizi lawama si kwa mimi tu, kuna
ambao alikuwa anaishi nao hapa Tandale, nao wamekuwa wakimlalamikia
kwamba siku hizi dogo ana dharau sana,” alisema Omar Jr, mkazi wa
Tandale Uzuri jijini Dar es Salaam.
Mama Masoud yeye ni mkazi wa Tandale-Chama jijini Dar es Salaam. Akimzungumzia Diamond kuhusu madai hayo, alisema:
“Mh! Ni kweli Diamond yule wa Tandale,
si huyu wa Madale (Dar). Mimi naona huyu wa Madale ana dharau sana si
kama zamani. Mimi nina kijana wangu walikuwa karibu zamani, lakini siku
hizi ukaribu haupo tena.
WAGOMA KUTUMIA BIDHAA ANAZOTANGAZA
“Diamond anapigiwa simu na kijana wangu
hapokei, si kama zamani. Mimi kwenye mapishi yangu nimeacha hata kutumia
ile bidhaa anayoitangaza kutokana na madharau yake.
“Tatizo nini unajua? Wabongo wengi
wakishapata pesa na jina kuwa kubwa, wanawadharau wote wa nyuma. Kumbe
basi mimi ninavyojua, kadiri mtu unavyopata pesa, ndivyo unavyotakiwa
kuzidisha unyenyekevu mbele ya watu, hasa wale wa chini ambao
wanakufahamu au wale waliyokua pamoja.”
MOHAMED SALUM, MKAZI WA TANDALE:
“Kiukweli maisha ya Diamond
yamebadilika, si kama zamani wakati hajatoka kisanii. Kwa sasa hawezi
kukaa akaongea na sisi watu wa chini zaidi ya kuongea na watu wenye
uwezo kama wake au zaidi.”
SHAFII HAMIS, MKAZI WA TANDALE:
“Ni hulka ya mwanadamu kubadilika kutoka
kwenye kipato cha chini na kuwa matawi. Mshikaji (Diamond) akija huku
anatusalimia kiaina, si kama zamani kipindi hajatoka na kwa sasa siyo
mkazi wa Tandale tena, ni wa Madale.”
AZIZI KUNAMBI, MKAZI WA TANDALE:
“Diamond kabadilika sana, si kama
zamani. Siku hizi anatudharau kwa sababu sisi hatuka kitu lakini sisi
ndiyo tuliyomlea mpaka alipofikia.”
MAMA ALI ‘MUUZA UBWABWA’, MKAZI WA TANDALE:
“Kwangu sijaona tatizo kwa kweli, akija
anaweza akasimama, akawasalimia washikaji au hata msosi wa hapa
mgahawani kwangu anaweza kununua na kula kama kawaida.”
IBRAHIM NASORO, MKAZI WA MADALE:
“Sisi tunaishi na Diamond lakini
hatumjui kwa sura zaidi ya kumwona kwenye tivii na magazeti. Kusema
ukweli ukisema nikwambie kama ni mwenzetu au la nitaku-danganya.
“Geti likifunguliwa anatoka akiwa ndani
ya gari. Akirudi anaingia akiwa ndani ya gari. Tunamwonea wapi! Angekuwa
mwingine alitakiwa kuwa beneti na sisi majirani, kwani kuna uzima na
ugonjwa sisi kama binadamu.”
MTANDAO ULIYOMTAJA
Hivi karibuni, Mtandao wa Forbes Africa
ulimtaja Diamond kuwa ni msanii ‘mwenye nazo’ barani Afrika kwa kumiliki
kitita cha shilingi bilioni nane za Kitanzania kwenye akaunti yake ya
benki, fedha anazozipata kwa shoo mbalimbali, ndani na nje ya Bongo.
Baada ya mtandao huo kuanika hesabu hiyo
ndipo baadhi ya watu walipoyatafsiri maisha ya sasa ya msanii huyo na
yale ya zamani, wakisema kwamba pesa inampa ‘kujisikia’.
APIGIWA SIMU NA GAZETI LA AMANI
Juzi, Jumanne, saa 8:20 mchana, gazeti
hili lilimpigia simu Diamond kwa lengo la kutaka kumsomea madai hayo
kisha kumsikia yeye anasemaje, lakini simu yake iliita bila kupokelewa!
CHANZO: GPL

Post a Comment