Video: Chid Benz Adaiwa Kutoroka Sober House
Msanii wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’.
DAR ES SALAAM: Wakati wadau wa
muziki wakifahamu kuwa Msanii wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo
‘Chid Benz’ yuko katika kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya
kulevya ‘sober house’ kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani, inadaiwa jamaa
alishatoroka kitambo na sasa yuko kitaa.
Taarifa iliyotua kwenye meza ya dawati
hili ilidai kuwa, Chid alitoroka kituoni hapo baada ya kushindwa
kuhimili mazingira yalikuwepo hivyo akaona bora arudi mtaani kwa staili
ya liwalo na liwe.
Baada ya kupata taarifa hiyo, mwishoni
mwa wiki iliyopita waandishi wetu walitinga Bagamoyo na kukutana na
meneja wa kituo hicho, Tumaini Majura ambaye alithibitisha kuondoka kwa
Chid akiwa bado anaendelea kupatiwa matibabu. Sehemu ya mahojiano kati
ya Risasi na meneja huyo ni hii;
Tumaini: Ni siku 28 lakini alitakiwa kukaa kwa muda wa angalau miezi mitatu ili kurudi katika hali yake ya kawaida.
Risasi: Ilikuwaje sasa mpaka akaondoka kabla hajawa sawa?
Tumaini: Nafikiri ni
uamuzi wake binafsi maana siku moja meneja wake (Babu Tale) alikuja
kumjulia hali, alipotaka kuondoka aling’ang’ania kuondoka naye. Sisi
pamoja na Tale tulimsihi sana kubaki lakini alikataa.
Risasi: Hali ilikuwaje kwa meneja wake wakati Chid anang’ang’ania juu ya jambo hilo?
Tumaini: Kiukweli
hakuwa akitaka aondoke maana mara kwa mara alikuwa anamsihi kuwa
mvumilivu ili amalize angalau miezi mitatu na ampeleke kwenye shoo za
muziki ndani na nje ya nchi, lakini Chid hakujali hayo. Kwa hiyo siwezi
kusema alifurahia juu ya jambo hilo.
Risasi: Maisha yake ya kawaida yalikuwaje na wenzake?
Tumaini: Hayakuwa
mabaya sana japo alikuwa mzito kushiriki kwenye ishu za usafi na vitu
vingine. Muda mwingi alipenda kupumzika na kuandika mistari. Lakini kuna
kipindi alikuwa akijaribu kuhamasisha wenzake wagomee kitu fulani. Sisi
tulikuwa tunamchukulia kama mtu wa kawaida aliyekuwa anahitaji msaada
kutoka kwa viongozi.
Baada ya mahojiano hayo, waandishi wetu
waliamua kumtafuta Chid Benz, alipopatikana alikataa kuzungumzia suala
hilo huku akisisitiza kuwa lolote kuhusu yeye atafutwe Babu Tale.
Alipopatikana, Babu Tale alisema:
“Sitaki kusikiliza wala kuzungumza lokote kuhusu Chid, muda ukifika
nitaongea ila kwa sasa niacheni tu.”
CHANZO: Boniphace Ngumije na Mayasa Mariwata, RISASI

Post a Comment