WAZEE WA YANGA WACHARUKA, WATAKA UCHAGUZI WA VIONGOZI USOGEZWE MBELE

Yanga wanaomba uchaguzi wao wa viongozi uliotangazwa, usogezwe mbele.
Wazee
wa klabu ya Yanga, umeomba mchakato wa uchaguzi mkuu wa timu hiyo
kusogezwa mbele hadi Julai 5, mwaka huu huku Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) ligomea maombi hayo.
Yanga
awali, iliagizwa na TFF, Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuanza
mchakato huo wa uchaguzi Mei 5, mwaka huu siku ambayo zoezi la utoaji
fomu kwa wagombea likianza.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wazee wa timu hiyo, Yahaya Akilimali alisema wanaheshimu
vyote vinavyosimamia soka na michezo ambavyo ni TFF na BMT ambavyo
wangependa kushirikiana navyo kwa manufaa ya klabu yao, lakini
wameviomba vyama hivyo kusogezwa mbele uchaguzi huo.
Akilimali
alisema, sababu inayowafanya kuomba uchaguzi usogezwe mbele ni vita
kubwa ya kupambana kutetea taji lao la Ubingwa wa ligi kuu, Fainali ya
FA na Kombe la Shirikisho Afrika (Caf) walipangwa kuvaana na Esperanca
ya Angola kati ya Mei 6-8, mwaka huu.
Aliongeza
kuwa, kwa hatua hii ya ligi kuu iliyofikia ni ngumu, hivyo wanatakiwa
kuzielekeza nguvu zao kwenye ligi kuhakikisha wanafanikisha malengo yao
waliyojiwekea kwenye msimu huu.
“Kwa
hatua hii tuliyofikia ya ligi kuu, tunahitaji mshikamo na umoja ndani
ya timu yetu ya Yanga na siyo kutengana kwa kutengeneza makundi ya
upinzani au kuanza kuonyesheana vidole.
“Kama
mnavyojua mechi zenyewe zimebaki tano tu za kumaliza ligi kuu, hivyo
tunawaomba TFF na BMT kama wanaosimamia soka na michezo kwa pamoja,
tunawaomba wasogeze mbe mchakato huu wa uchaguzi wa Yanga,” alisema
Akilimali.
Alipotafutwa
Mwenyekiti wa Uchaguzi wa TFF, Aloyce Komba kuzungumzia hilo alisema
“Kabla maombi hayo hayajafika kwenye meza yangu, ningewaambia tu hao
Yanga, hilo suala halipo na tarehe ya uchaguzi haitabadilika.
“Yanga
ratiba hiyo wanaijua vizuri kwa sababu tulishamtaarifu katibu wao
Baraka (Deudedit), hivyo tunashangaa hayo mengine yanatoka wapi,
tunawaambia kuwa wao wanatakiwa wajipange vizuri kwa kucheza mechi za
ligi kuu, Fainali ya FA na michuano hiyo ya kimataifa.
“Sitaki
kutumbuliwa na mimi kama hao viongozi wengine wanavyotumbuliwa,
serikali ipo makini hivi sasa katika masuala haya,” alimalizia Komba.
Post a Comment