TORRES ASEMA ATLETICO MADRID IKO TAYARI KUANDIKA HISTORIA DHIDI YA BAYERN
Mshambuliaji
wa Atletico Madrid, Fernando Torres amesema kikosi chao kilo tayari kwa
mechi ngumu ya leo dhidi ya Bayern Munich.
Nusu
fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, inasubiriwa kesho kwa hamu
kubwa jijini Madrid lakini Torres amesema wake tayari kuandika historia
nyingine.
“Tuko tayari kuandika historia mpya, tuko tayari kupambana na tunaisubiri siku hiyo kwa hamu,” alisema Torres.
Atletico ambayo imesherekea miaka 113 tokea kuanzishwa kwake imekuwa moja ya timu tishio katika kipindi hiki.
Nusu fainali ya kwanza, imechezwa leo na Real Madrid ikiwa ugenini imepata sare ya 0-0 dhidi ya Manchester City.

Post a Comment