Mapokezi Ya Rais Wa Sudan Salva Kiir Ikulu Jijini Dar Es Salaam Na Utiaji Wa Saini Kujiunga Na Jumuiya Ya Afrika Mashariki
Rais
wa Sudan Kusini Mhe. Jenerali Salva Kiir leo ametia saini mkataba wa
nchi yake kujiunga rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Kiir ametia saini mkataba huo leo Jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Viongozi
wa nchi za jumuiya hiyo waliidhinisha kukubaliwa kwa Sudan Kusini
kujiunga na jumuiya hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika mjini Arusha
mwezi uliopita.
Sudan
Kusini itakuwa nchi ya sita kujiunga na Jumuiya hiyo iliyoanza kwa nchi
tatu za Tanzania, Kenya na Uganda kabla ya Rwanda na Burundi kujiunga
na jumuiya hiyo baadaye.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) akiwa na Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan
katikati na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa wakimsubiri Rais
wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir
alipowasili Ikulu na kupokelewa na kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa
kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit
wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa
kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit
wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa
kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016, Kushoto ni
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit akikagua gwaride la heshima wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu leo.
Rais
wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir
akiwapungia mikono viongozi mbalimbali huku akiongozana na mwenyeji wake
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakati
alipowasili Ikulu

Post a Comment