MADIWANI WA CUF, CHADEMA WASHINDA KESI
Diwani wa Kata ya
Manzese (Cuf), Ramadhan Kwangaya akihojiwa na wanahabari nje ya Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu leo, Aprili 29, 2016.
Diwani wa Kata ya
Gongolamboto, Jacob Kissy akizungumza na wanahabari mara baada ya hukumu
kutolewa, nje ya Mahakama ya Kisutu leo.
Baadhi ya
wafuasi wao wakiondoka mahakamani hapo
baada ya ushindi huo.
MADIWANI wa
upinzani kupitia Chama Cha Wananchi (Cuf), Ramadhan Kwangaya (Manzese) na Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jackob Kissy (Gongolamboto) jijini Dar,
leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu wameshinda kesi zilizofunguliwa dhidi
yao na waliokuwa wagombea udiwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) za kupinga
matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
Akizungumza na waandishi
wa habari nje ya mahakama hiyo, Kwangaya alisema mpinzani wake alifungua kesi
akimtuhumu kwamba katika uchaguzi huo, alifanya fujo katika kituo cha kuhesabia
kura, kura zaidi ya elfu moja hazikuhesabiwa na kwamba baadhi ya wasimamizi wa
vituo walitumia lugha ya Kiingereza kwa wapiga kura wao.
Kwa upande wa Kissy,
aliwaambia waandishi wa habari kwamba amefurahishwa na maamuzi yaliyotolewa na mahakama na kwamba
haki imetendeka. Kesi hizo zilikuwa zikisikilizwa na hakimu wa mahakama hiyo,
Lita Tarimo.
Post a Comment