Kajala amtolea chozi kigogo wa wema!
Na Imelda Mtema
Siku chache baada ya gazeti dada na hili, Risasi Jumamosi kuandika juu ya aliyekuwa kigogo wa msanii Wema Sepetu, Clement Kiondo ‘CK’ kunaswa akiuza mishikaki, tukio hilo limemliza shosti wa Wema, Kajala Masanja.
Siku chache baada ya gazeti dada na hili, Risasi Jumamosi kuandika juu ya aliyekuwa kigogo wa msanii Wema Sepetu, Clement Kiondo ‘CK’ kunaswa akiuza mishikaki, tukio hilo limemliza shosti wa Wema, Kajala Masanja.
Kumwaga
chozi kwa Kajala kumetokana na maelezo yake kwamba, baada ya kuiona
habari hiyo hakuweza kuamini kama kweli ni CK yule aliyewahi kumtolea
shilingi milioni 13 kama faini ili asiende jela kutokana msala aliokuwa
nao.

Kajala Masanja

Wema Sepetu
Akizunbumza
na Ijumaa kwa majonzi, Kajala alisema: “Kiukweli nililia sana,
nilishindwa kuamini kama kweli CK amefikia hali hiyo,” alisema Kajala
ambaye pia aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na jamaa huyo.
Akasema
stori hiyo isingekuwa imeambatana na picha asingeamini lakini alipoona
zile picha zinazomuonesha CK akiwa jikoni akimhudumia mtu, alishindwa
kujizuia na kujikuta akibubujikwa na machozi.
Tukio la kunaswa kwa
CK akiuza mishikaki lilinaswa na mapaparazi wetu juzikati kwenye baa
moja iliyopo maeneo ya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, jambo
lililozua maswali mengi kutokana na jeuri ya fedha aliyokuwa nayo kigogo
huyo. FUNGUA HAPA KUJIONEA ALIVYONASWA AKIUZA MISHIKAKI ===> HAPA BONYEZA
CHANZO: IJUMAA
Post a Comment