Bunge, PAC wavutana uchunguzi wa Lugumi
SAKATA la mkataba wa Jeshi la Polisi na
kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd, limechukua sura mpya baada ya hadidu rejea
zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) kwa
kamati ndogo iliyoundwa ajili ya kuchunguza mkataba huo, kutofautiana na za
Bunge.
Mkataba uliozua utata, uliingiwa mwaka 2011 baina ya jeshi
la polisi na kampuni ya Lugumi, kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukulia
alama za vidole kwenye vituo vya polisi 108, lakini hadi sasa imefunga vituo 14
na kulipwa Sh. Bilioni 34, sawa na asilimia 99 ya fedha zote, kinyume cha
Sheria ya Ununuzi wa Umma.
Baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu, Aprili 23, mwaka
huu, PAC ilikutana na kuteua wajumbe tisa watakaounda kamati ndogo kuchunguza
sakata hilo kwa undani na kuandaa hadidu za rejea za kufanyia kazi.
Baadhi ya adidu za rejea zilizojadiliwa na PAC ni pamoja na kuangalia thamani ya vifaa vilivyonunuliwa na hali halisi ya soko na kama kulikuwa na ulazima wa kutoa kazi hiyo kwa mbia mmoja.
Baadhi ya adidu za rejea zilizojadiliwa na PAC ni pamoja na kuangalia thamani ya vifaa vilivyonunuliwa na hali halisi ya soko na kama kulikuwa na ulazima wa kutoa kazi hiyo kwa mbia mmoja.
Pia kamati hiyo ilitakiwa kuangalia kama Lugumi ililipa
kodi katika fedha ilizolipwa kutokana na mkataba huo. Nyingine ni kupitia mfumo
mzima wa utoaji zabuni ikiwa ni pamoja na nyaraka za zabuni alizopewa mzabuni
na zile alizojaza, kuangalia uwezo wa kampuni kama ilikuwa na sifa za kupewa
kazi hiyo.
Siku moja baada ya kufanyika kwa kikao hicho cha PAC na
kutangaza majina ya wajumbe wa kamati ndogo, Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa kwa
umma ambayo ilisema kamati hiyo ndogo itajigawa kwenye makundi matatu na kupita
kwenye maeneo husika kuhakiki kazi iliyopewa.
“.. Kwa mujibu wa hadidu za rejea ambayo ni kufanya
uhakiki iwapo vifaa vinavyohusiana na mradi ulioingiwa kati ya jeshi la polisi
na kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd, kuhusu ufungaji wa vifaa vya utambuzi wa
alama za vidole, vilinunuliwa na vilifungwa katika maeneo husika,” inasema
sehemu ya taarifa hiyo.
Akizungumza na Nipashe jana, Naibu Katibu wa Bunge, John
Joel, alisema hoja ya CAG ilikuwa kufungwa kwa vituo vifaa hivyo kwenye vituo
14 badala ya 108, jambo ambalo ndilo linalotakiwa kufuatiliwa na kamati hiyo
ndogo na si vinginevyo.
Alisema kwa sasa suala la sakata la Lugumi
linavyochukuliwa ni sawa kwamba kuna mtu anatafutwa, jambo alilosema halipaswi
kuwa la Bunge bali mtu anayedhani ana kitu chake binafsi anatakiwa kuwasilisha
hoja binafsi bungeni.
“Kukagua kampuni imesajiliwa na vitu vingine si kazi yao.
Hiyo inahusiana na hoja ya ukaguzi aliyoitoa CAG? Kama haihusiani na hoja ya
CAG hiyo kazi nyingine wanaipata wapi wao? Hoja ya ukaguzi inasema ni kufunga
mashine kwenye vituo, sasa wao wanaenda kuchunguza kampuni si ajenda ya CAG
tena?
“Kwani wao (PAC) wanachotaka sasa hasa ni nini? Maana
mnataka kutuchanganya ninyi waandishi wa habari,” alisema Joel na kuongeza
kuwa: “Wanachokwenda kufanya ni kitu gani, kama wanataka kwenda kufanya kazi
hiyo (kukagua kama vifaa hivyo kama vimefungwa au la), manake sasa wanakwenda
kinyume kwa sababu hiyo haikuwa hoja ya CAG, kwa maana hiyo wao wananzisha hoja
yao.
“Hiyo ya kampuni kama ni halali, si halali, imelipa kodi
haijalipa kodi, hayo yanatoka wapi? Kwa sababu ingekuwa ndiyo hoja ya CAG
ingekuwa sawa. Kama si hoja yake manake sasa kamati inatakiwa ilete taarifa
bungeni itoe hoja kwamba kuna kitu fulani halafu Bunge sasa liwakubalie kwamba
nendeni mkatuchunguzie hayo mambo.”
Alisema kwa sasa PAC haijatoa taarifa bungeni “halafu
inaanza kutafuta kazi? Hiyo si sawa, kwa sababu kamati ile inatakiwa ifanye
kazi kwa mujibu wa kanuni.
“Lazima inapokuwa inafanya kazi iangalie majukumu yake na
mipaka yake ya kazi, na najua spika amewapa ruhusa ya kuunda hiyo kamati ndogo
na amewapa adidu za rejea ni kitu gani cha kwenda kufanya.
“Wakienda huko wakagundua mambo mengine inatakiwa yaje
yaombewe kibali bungeni kwa sababu siyo sehemu ya ripoti ya CAG, na kama
wanakwenda kufanya hiyo kazi nyingine hakuna sababu ya kumuhusisha CAG wala
hazina, wala hata polisi kwa sababu sasa hapo polisi au wizara ya mambo ya
ndani inahusika nini kwenye masuala kama hayo?
“Jinsi hii hoja inavyojengwa inajengwa kwa minajili
kwamba kuna mtu anatafutwa, kama kuna mtu anatafutwa hiyo isiwe ni issue
(jambo) ya Bunge. Ingekuwa issue ya individual (liwe suala binafsi) wakaileta
kama hoja binafsi ama waka watavyotaka kufanya lakini kama ni hoja ya CAG
wasiweke vitu vingine ambavyo CAG hakuhoji,” alisema Joel.
Makamu Mwenyekiti.
Makamu Mwenyekiti.
Alivyotafutwa kutolea ufafanuzi suala hilo, Makamu
Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilary, alisema kwa sasa kazi ya kufanya uchuguzi huo
ameiacha kwa kamati ndogo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ndogo ambaye ni Mbunge wa
Same Mashariki (Chadema), Naghenjwa Kaboyoka, aliliambia gazeti hili kuwa mpaka
sasa hawajapata hadidu za rejea kutoka Ofisi ya Spika na kuwa wakishakabidhiwa
ndiyo watajua nini cha kufanya.
“Lakini kama uambiwe uende Dodoma ukaangalie kama bungeni
pale komptuta zilikuwa zimewekwa, lazima ujue mkataba ulitaka ziwekwe ngapi na
za aina gani. Details (undani) haziwezi kuandikwa kila mahali. Ni sawa na
kufanya utafiti, huwezi kuandika kila kitu lakini kama unavyoenda maswali
yanaibuka na vitu vingine ndiyo unapata picha halisi.
“Huwezi kwenda kuchunguza bila kujua unachunguza kitu
gani. Lazima uambiwe na si kuambiwa tu kwa maneno,
utaenda kuangalia nini? Unaambiwa uchunguze magari 10, kwa nini unachunguza? Ni kwa sababu kuna tuhuma, kwa hiyo lazima uangalie mkataba unasemaje? Kama umeambiwa 10 mkataba kweli ulikuwa unasema 10 au 15, kwa hiyo mimi nafikiri kutakuwa hakuna tatizo,” alisema Kaboyoka.
utaenda kuangalia nini? Unaambiwa uchunguze magari 10, kwa nini unachunguza? Ni kwa sababu kuna tuhuma, kwa hiyo lazima uangalie mkataba unasemaje? Kama umeambiwa 10 mkataba kweli ulikuwa unasema 10 au 15, kwa hiyo mimi nafikiri kutakuwa hakuna tatizo,” alisema Kaboyoka.
Alisema kamati ndogo ikikaa ndiyo itaangalia hadidu za
rejea na kisha waone ni nini cha kufanya.
“Unajua uchunguzi inategemea malengo yenu ni nini, je taarifa tuliyo nayo itakuja kutusaidia tunachotaka, utakuja kuandika ripoti gani?
“Unajua uchunguzi inategemea malengo yenu ni nini, je taarifa tuliyo nayo itakuja kutusaidia tunachotaka, utakuja kuandika ripoti gani?
“Kama vimefungwa ni vingapi? Utathibitisha nini maana
unaweza kuambiwa taarifa ambayo hujui kama ndivyo mkataba ulivyokuwa unasema na
ukatoa taarifa ambayo umeegemea kwenye kitu ambacho hakikuwa sahihi, wewe
unaonekana umefanya ile kazi hukuwa makini.
“Ni sawa na uambiwe ukachunguzi ni watoto wangapi
wameolewa na umri mdogo, kwani sheria inasema? Lazima uijue, anatakiwa aolewe
na umri gani? Lazima uwe na sheria ile.
“Maana vinginevyo utakuwa uncheza tu, lazima upate
maelezo ya kila kitu, unapofikia daraja ndo unajua hili daraja naweza kulikwepa
ama linaweza kubeba gari langu?” alisisitiza.
Hivi karibuni gazeti hili lilibaini kuwa ajenda ya
kukabiliana na ugaidi ilitumika kuidhinisha zabuni hiyo na kuvunjwa kwa sheria
za manunuzi.
Mpango huo ulisukwa baada ya baada ya Bunge kupitisha
bajeti ya Wizara ya Mambo ya ndani kwa mwaka 2011/12, ambayo ndani yake ilikuwa
na kipengele cha ununuzi wa vifaa maalum (specialized equipment).
“Kutokana na hali ya wakati huo ambapo matukio ya uhalifu
wa kutisha na viashiria vya ugaidi vilivyokuwa vimeanza kujitokeza, jeshi la
polisi liliamua kununua mfumo utakaotumika katika utambuzi wa alama za vidole.
Ununuzi wa mfumo huo ulikuwa muhimu kwa jeshi la polisi
kwa ajili ya kuimarisha usalama wa nchi, raia na mali zao
Kwa kuzingatia unyeti wa kazi iliyotegemewa kufanyika kwa mfumo huu ilibidi kutumia njia ya single source (kutumia mdhabuni mmoja bila kushindanisha wengi apatikane mmoja bora) hivyo jeshi la polisi lilikaribisha Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kufunga mfumo huo,” inasema sehemu ya taarifa hiyo ambayo Nipashe imeiona.
Kwa kuzingatia unyeti wa kazi iliyotegemewa kufanyika kwa mfumo huu ilibidi kutumia njia ya single source (kutumia mdhabuni mmoja bila kushindanisha wengi apatikane mmoja bora) hivyo jeshi la polisi lilikaribisha Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kufunga mfumo huo,” inasema sehemu ya taarifa hiyo ambayo Nipashe imeiona.
Inaeleza kuwa, kwa kuzingatia matakwa ya sheria ya
Ununuzi wa Umma ya mwaka 204, polisi kupitia kitengo chake cha PMU, lilianzisha
mchakato wa mfumo huo.
Taarifa hiyo inasema kuwa, Septemba 16, 2011, bodi kasimu
ya jeshi la polisi iliidhinisha uanze mchakato wa ununuzi ya mfumo huo kwa
kutumia njia hiyo ya ‘single source’ na kisha kampuni ya Lugumi ikapewa nyaraka
za zabuni.
Inaeleza kuwa Septemba 22, mwaka huo ufunguzi wa zabuni
hiyo ulifanyika ambapo uliudhuriwa na mwakilishi wa
Kampuni ya Lugumi.
Taarifa hiyo inasema, simu iliyofuata (Septemba 23) Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, aliteua kamati ya tathmini iliyokuwa na wajumbe watano.
Taarifa hiyo inasema, simu iliyofuata (Septemba 23) Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, aliteua kamati ya tathmini iliyokuwa na wajumbe watano.
Siku saba baadaye (Septemba 29), kamati ya zabuni
iliwasilisha ripoti ya tathimini ambayo ilipendekeza Kampuni ya Lugumi
Enterprises.
Ilipofika Novemba 8, taarifa hiyo inasema bodi kasimu ya
zabuni ya jeshi la polisi, ilifanya kikao na kuridhia mapendekezo ya kamati ya
tathimini kwa kuiteua kampuni ya Lugumi Enterprises.
Baada ya mchakato huo, taarifa hiyo inasema Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, aliidhinisha wizara kuingia mkataba na Lugumi kwa barua yenye
kumbukumbu namba JC/A/130/11/1 iliyoandika Novemba 25, 2011.
Licha ya kuharakishwa kwa mchakato wa kumpata mzabuni bila
kumshindanisha au kujiridhisha na uwezo wake wa kuleta vifaa bora, taarifa hiyo
ya polisi inasema mpaka leo ikiwa ni takribani miaka mitano tangu mzabuni
alipopitishwa, kwenye baadhi ya maeneo vifaa hivyo havifanyi kazi.
Taarifa hiyo inasema kwenye maeneo mengi vifaa hivyo
havifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa mfumo wa mtandao wa intaneti.
Hali iyo inandelea kuzusha maswali mengi ikiwa ni pamoja
na je, kwa nini walinunua vifaa vinavyotegemea mfumi huo pekee na kupanga
kuvifunga nchi nzima ilihali walijua kabisa hali ya upatikanaji wa mtandao
nchini?
Kwa muda mfupi uliotumika kumpata mzabuni bila
kumshindanisha, ni kigezo gani kilitumika kuiteua kampuni ya Lugumi Enterprises
na siyo nyingine yoyote?
Ikiwa ni miaka takribani sita sasa tangu fedha za kununua
vifaa hizo kutolewa na kwenye maeneo mengine bado havijafungwa, viashiria vya
ugaidi vilivyotajwa kuwa moja ya sababu ya kuharakisha ununuzi wa vifaa hivyo
vimeishia wapi? Ajenda hiyo ilitumika kubariki utolewaji wa fedha haraka?
CHANZO; NIPASHE

Post a Comment