AZAM TV YAFANYA KWELI, YAZINDUA KIWANDA CHA FILAMU
AZAM
TV kupitia chaneli yake ya Sinema Zetu, mapema leo imezindua rasmi
‘projekti’ iliyopewa jina la Kiwanda cha Filamu, na kipindi kipya
kiitwacho Taxi, vyenye lengo la kuibua vipaji vya wasanii wa maigizo
na wapiga picha za video chipukizi.
![]() |
Meneja Masoko na Mauzo wa Azam Media, Mgope Kiwanga, akifafanua zaidi namna projekti hiyo itakavyonufaisha watu wengi. |
Projekti
hiyo ambayo ilianzishwa mwanzoni mwa Machi mwaka huu ilitoa furasa kwa
watu mbalimbali ambao wangependa kushiriki kutuma kazi zao na
wamepatikana zaidi ya washiriki 200.
Akizungumza
na wanahabari katika uzinduzi huo kwenye ofisi za Azam zilizoko eneo la
Tazara jijini Dar, Msimamizi wa Uzalishaji wa Sinema Zetu, Zamaradi
Nzowa, alisema washiriki hao watawachuja chini ya majaji akiwemo
muigizaji wa siku nyingi hapa nchini, Suzan Lewis ‘Natasha’, ili
kuwapata washiriki 22.
Baada
ya kupatikana, watapatiwa mafunzo mafupi kisha wao pamoja na mastaa wa
filamu hapa nchini watashiriki kwenye tamthilia itakayojulikana kwa jina
la Taxi.
![]() |
Muigizaji Suzan Lewis ‘Natasha’, (kushoto) akimlisha keki msanii na mtangazaji mahari Bongo, Daniel Kijo. |
Nzowa
alisema: “Washiriki ni kuanzia umri wa miaka 18 na kesho Jumatano pale
Coco Beach ndipo tutaanza kufanya mchujo wa awali ambapo mpaka mwisho
tunatarajia kupata waigizaji 20 na wapiga picha wawili ambao watashiriki
kwenye tamthilia ya Taxi ambayo itazinduliwa Julai mwaka huu na itakuwa
ikionyeshwa katika chaneli yetu ya Sinema Zetu.”
![]() |
Mwandishi wa gazeti la Championi, Mohamed Mdose (kushoto) akilishwa keki na Natasha. |
Post a Comment