AHLY WAPANGA KUIPELEKA YANGA NJE YA MJI WA CAIRO, YAELEZWA MECHI NI ALEXANDRIA
Wakati
Yanga inaondoka leo kwenda Cairo nchini Misri kuivaa Al Ahly, dalili
zinaonyesha mechi hiyo lazima itachezwa kwenye mji wa Alexandria.
Alexandria
ni mji ulio kaskazini mwa nchi ya Misri na mwaka juzi Yanga walicheza
kwenye uwanja wa jeshi wakati walipoivaa Al Ahly.
Inaonekana
bado hakuna usalama wa kutosha katikati ya jiji la Cairo, hivyo mechi
hiyo inaweza kupelekwa Alexandria na sasa tayari ni asilimia 90
haitachezwa Cairo.
"Hawasemi
vizuri lakini taarifa tulizonazo kuwa mechi ni Alexandria na si Cairo.
Hivyo watu wakija lazima watasafiri tena kwa takribani saa tatu hadi nne
kwenda Alexandria," alisema Mtanzania anayeishi Cairo.
"Unajua bado wana hofu ya usalama, ingawa kuna taarifa kwamba ile mechi dhidi ya Nigeria inawapa matumaini kuwa watu watatulia."
Katika
mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, Yanga ilitoka sare ya bao 1-1,
hivyo inalazimika kushinda au sare ya kuanzia mabao mawili na kuendelea.

Post a Comment