Mrembo Naj Athibitisha Uhusiano Wake na Barakah Da Prince Kwa Picha Hii
Naj hataki kuficha tena penzi lake na muimbaji wa ‘Siwezi’, Barakah Da Prince.
Uhusiano
wao ambao hauna muda mrefu tangu uanze, unaonekana kukolea siku hadi
siku. Naj amepost picha Instagram ya kichwa cha Barakah huku mkono wake
wenye kucha zilizopakwa rangi ya njano ikikikishika.
Ni
hivi karibuni tu pia Barakah alidai kumpata mpenzi anayeamini kuwa
ndiye aliyeushika moyo wake. Japo picha ya msichana aliyekuwa kwenye
picha yake haikuonesha sura yake, msuko aliokuwa nao ulithibitisha kuwa
alikuwa ni Naj.


Post a Comment