MR BLUE, TUNDAMANI, KHADIJA KOPA,MSAGA SUMU KUKINUKISHA MWEMBE YANGA JUMAMOSI HII!
WASANII
wa muziki mbalimbali hapa nchini, Jumamosi hii wanatarajiwa kukinukisha vilivyo
katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam, katika tamasha la Amsha
Mama Festival.
Akizungumza
kwa niaba ya wasanii wenzake, Balozi wa tamasha hilo Khalid Ramadhani ‘Tundaman’, ambaye amepewa
Ubalozi huo kupitia waandaaji wa tamasha
la (AFWAB) AMSHA MAMA Festival 2016, lililo
chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa lebo ya Candy na Candy Records
Joe Kariuki, alisema tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Machi 5 mwaka huu katika
uwanja wa Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Tundaman
na Muandaaji wa tamasha hilo Kariuki, wamesema kwamba maandalizi ya shoo hiyo
tayari yameshakamilika kwa kiasi kikubwa hivyo angependa kutumia fursa hii
kuwaalika wakazi wote wa jiji la Dar, kujumuika siku hiyo kushuhudia burudani
mbalimbali zitakazotolewa na wasanii kibao ambao tayari wemedhibitisha kufanya
makamuzi siku hiyo.
“Tunapenda
kuwaalika Watanzania wote kwa ujumla siku ya jumamosi hii ya Machi 5, mwaka huu
waje kwa wingi katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar Salaam, ili tujumuike kwa pamoja katika
tamasha la kuhamasisha wanawake kujikwamua katika shughuli zao mbalimbali za
kiuchumi.
Tamasha
hili litakuwa ni la wazi kwa maana kwamba watu wote watapata burudani kibao
bila malipo yaani bure kabisa hivyo waje kuwashuhudia wasanii kama, Khadija
Kopa, Mr Blue, Snura, Msaga Sumu, Ali Chocky na Tunda Man wakitoa burudani ya
hali ya juu kwani ulinzi na usalama siku
hiyo ni wa uhakika,” alisema Tunda Man.
Kwa
upande wake, Joe Kariuki ambaye ni
mratibu mkuu wa
tamasha hilo ametumia muda huu kuongea na baadhi ya akinamama
wanaojishughulisha na biashara za vitu mbalimbali hususani mama ntilie, wauza
matunda na wauzaji wa mitumba ili nao wajitokeze kwa wingi kuja kunadi bidhaa
zao siku hiyo kwani hiyo ndiyo fursa yao
ya kipekee ya kujitangaza bure.
Post a Comment