ad

ad

HAYA NDIYO MANENO ANAYODAIWA ISIHAKA KUMTUPIA MAYANJA ALIPOTAKA ACHEZE DHIDI YA SINGIDA UNITED





Simba imetangaza kumsimamisha nahodha wake, Hassan Isihaka baada ya kudaiwa “kumtemea mbovu” kocha wake Jackson Mayanja.

  Wadau wanasema  kwamba, Mayanja ambaye alimuacha katika kikosi chake beki huyo wakati Simba ilipoivaa Yanga, aliamua kumpanga katika mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United.

Inadaiwa, Isihaka baada ya kuambiwa atacheza, mbele ya wachezaji wenzake, alimuuliza Mayanja hivi: 

“Kwani likizo yangu ya kukaa benchi imeisha lini, uliona siwezi kucheza na Yanga, ila naweza kucheza leo.”


Inadaiwa, kauli hiyo inaelezwa kuwashangaza wengine, lakini Mayanja akaamua kuachana naye na kumpanga  Lufunga, beki mpya aliyejiunga wakati wa dirisha dogo akitokea African Sports. Simba ilishinda kwa mabao 5-1 na kutinga robo fainali.

No comments

Powered by Blogger.