HAJI MANARA AKANUSHA TAARIFA YA MECHI YA COASTAL VS SIMBA KUAHIRISHWA
| MANARA |
Mkuu
wa kitengo cha Habari cha Simba na Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara
amekanusha taarifa kwamba alitoa taarifa kuwa mechi ya Coastal Union
dhidi ya Simba wikiendi hii imeahirishwa.
Manara amesema ni uzushi ambao unasambazwa na watu wasiojulikana wenye nia ya kutaka kuwachanganya Wanasimba.
"Si
kweli, mtu kaweka tu kwa makusudi sijui nia yake ni nini. Anataka
kuwachanganya Wanasimba na huenda wanachanganywa na ushindi mfululizo wa
Simba jambo ambalo hawalifurahii," alisema Manara alipozungumza na
SALEHJEMBE.
"Ukweli mechi ipo na kikosi kinaendelea na maandalizi kama kawaida," alisisitiza.
TAARIFA ALIYOTOA MANARA KUKANUSHA:
Napenda kukanusha hyo taarifa inayotembea mitandaoni ikihusisha jina langu.eti mechi yetu imehairishwa.
Ni uongo unaozushwa na wapinzani wetu wanaotapapa na matokeo yetu kwa sasa.
Puuzen taarifa hyo.ni ujinga na ulofa uliochupia mpaka.
Haji manara
Simba nguvu moja
TAARIFA INAYOELEZWA KUWA NI YA UZUSHI:
Habari
wanachama na mashabiki wa SIMBA, kwa sasa timu yetu iko vizuri na mungu
akipenda huu ndio mwaka Wa mwisho wa sisi kuitwa wa mchangani, hivyo
nawaomba muisapoti timu yetu popote iendapo,
Napenda
kuwapa official taarifa kuwa mechi iliotakiwa ichezwe tarehe 19 march
2016, Dhidi ya COSTAL UNION, HAITAKUWEPO, mechi hii imekuwa postponed
mpaka TFF watakapo tangaza itachezwa lini, hivyo wanachama wenzangu
msije kupoteza nauli zenu bure kwenda TANGA, NARUDIA TENA MECHI
HAITAKUWEPO, sambaza ujumbe huu kwa GROUP zote ulipo,
SIMBA NGUVU MOJA
Imetolewa na Mimi Afisa habari wanu
Hajji S. Manara
Post a Comment