Taarifa ya Uteuzi wa MKurugenzi MKuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amemteua
Hamza Said Johari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Nchini (TCAA).
Taarifa
ya uteuzi huo imetolewa na Katibu Mkuu (Uchukuzi), Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leornald Chamurinho ambapo imeeleza kuwa
uteuzi huo unaanza Februari 22 mwaka huu.
Kabla
ya uteuzi huo, Johari alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Walaji wa
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA – Consumer Consultative
Council).
Mkurugenzi Mkuu huyo mteule amejaza nafasi iliyokuwa ikikaimiwa na Redemptus Bugomola.

Post a Comment