NILIUA KUMLINDA MAMA YANGU (I Killed to protect my mom) - 02

ILIPOISHIA
Edson huyu waliyekutana naye hakuwa yule wa nyuma. Alizaliwa kwenye familia ya kitajiri, alikulia huko ila baada ya wazazi wake kufariki, mali zote zilikwenda kwa ndugu zake waliokuwa na tamaa na yeye kumuacha.
Edson huyu waliyekutana naye hakuwa yule wa nyuma. Alizaliwa kwenye familia ya kitajiri, alikulia huko ila baada ya wazazi wake kufariki, mali zote zilikwenda kwa ndugu zake waliokuwa na tamaa na yeye kumuacha.
Maisha yakampiga, nyumbani akafukuzwa na kukimbilia mitaani, huko,
alisulubika, alilia usiku na mchana, hakuwa na amani, wakati mwingine hata
kula, chakula chake kilikuwa cha shida mno.
Alipambana lakini akashindwa, akaanza kutafuta kazi za kufanya, kila
alipokwenda, kwa jinsi alivyoonekana hakukuwa na mtu aliyeamini kama mtu huyo
alikuwa raia mwema, alionekana mchafumchafu, alifanana na mhuni, mvuta bangi na
mbwia madawa ya kulevya. ENDELEA....
Baada ya kuteseka sana ndipo akafanikiwa kupata kazi katika kampuni
ya Mediteranian ambayo ilikuwa na boti zenye jina la Royal Palm ambazo zilikuwa
zikifanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar.
Huko, alikwenda kama mbeba mizigo. Japokuwa kipindi cha nyuma
aliiona kazi hiyo kuwa mbaya lakini kwa kipindi hicho, hiyo ilionekana kuwa
bora kuliko kukaa mitaani akiombaomba hela kwa kila rafiki yake aliyemuona.
Kidogo akapata ahueni, akapanga chumba maeneo ya Manzese na kuanza
maisha huko. Hakuwa na mshahara mkubwa, alipata kidogo na hichohicho ndicho
alichokitumia kuyatengeneza maisha yake.
Siku zikakatika, maisha yakaanza kuwa mazuri japo si sana. Kila siku
alihakikisha anafika kazini na kuanza kazi yake ya kubeba mizigo. Kwa
kumwangalia, ingekuwa vigumu kuamini kama mtu huyo aliwahi kuishi maisha ya
kitajiri kabla ya wazazi wake kufariki dunia.
Mara nyingi alikuwa akisafiri na boti mbalimbali kuelekea Unguja na
Pemba, huko, kama kawaida alikuwa na kazi ya kushusha mizigo na kupandisha,
ndiyo kazi ambayo aliizoea na ndiyo hasa iliyomuweka mjini.
Kutokana na maisha mabovu aliyokuwa nayo, hakukuwa na mwanamke
aliyetamani kuwa naye. Wanawake wengi walifikiria fedha, waliwafuata wanaume
wenye fedha hivyo kwa mtu kama yeye, hakukuwa na msichana aliyemfuata, tena
wengi walipomuona, walimdharau.
Moyoni aliumia, alitamani kuwa na heshima, alitamani kupendwa kama
watu wengine lakini hiyo haikuwezekana, hakuwa na uwezo wa kuwa na fedha,
hakuamini kama ingetokea siku angeweza kupata fedha.
Baada ya kupita miaka hiyo miwili ndipo akakutana na msichana wa
ndoto yake, msichana aliyempenda kuliko mtu yeyote yule, huyo alikuwa Anita,
msichana yule wa kipindi cha nyuma ambaye alimwambia kwamba alikuwa akimpenda
sana.
Leo hii, msichana huyuhuyu ambaye waliwekeana ahadi kwamba wangeoana
alikuwa na mwanaume mwingine, mwanaume mwenye sura ya kipole ambaye hakuonekana
kama alikuwa mtu katili, uso wake tu ulionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa
kwenye mapenzi ya dhati kwa mke wake.
“Mnakwenda wapi?” aliuliza Edson huku akimwangalia Anita machoni,
bado alihisi mapenzi mazito kwa msichana huyo.
“Tunakwenda Zanzibar....”
“Pemba au Unguja?”
“Unguja.”
“Waoo! Sawa! Nitahakikisha nawasaidia, hasa kubeba mizigo, tena bila
gharama yoyote ile,” alisema Edson huku akiachia tabasamu.
“Sawa! Tutashukuru sana,” alisema Anita.
Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, hakuamini kama yule
aliyekuwa akimwangalia alikuwa Edson, yuleyule mvulana aliyempenda sana tangu
walipokuwa shuleni.
Hali hiyo hakutaka mumewe aione, hakutaka kugundulika ila mara
nyingi alimwangalia kwa macho ya mahaba yalioonyesha kuwa na uhitaji wa kuwa na
mwanaume huyo.
Baada ya dakika kadhaa, abiria walipotimia ndani ya boti, ikawashwa
na safari ya kuelekea Unguja na Pemba kuanza huku Edson akiwa bize katika
sehemu ya kutunza mizigo.
****
“Yule ndiye Edson mwenyewe?” aliuliza Phillip.
“Ndiye yeye! Amekwisha sana, ni vigumu kuamini kama huyu ndiye yule
Edson niliyesoma naye,” alisema Anita huku akionekana kuhuzunishwa na hali
aliyokuwa nayo Edson.
“Ndiyo maana nimeshangaa, jinsi ulivyoniambia na jinsi alivyo, ni
vitu viwili tofauti kabisa,” alisema Phillip.
“Ndugu wamechukua kila kitu alichoachiwa na wazazi wake, anatia
huruma sana,” alisema Anita.
Muda huo, boti ilikuwa safarini, ilianza safari ya kuelekea Zanzibar
huku bahari ikiwa imetulia kabisa. Ndani ya boti ile kila mmoja alikuwa bize
kuzungumza na mwenzake, walitegemea kutumia saa moja baharini mpaka kufika
Zanzibar.
Kadiri muda ulivyozidi kwenda na ndivyo idadi ya watu waliokuwa
wakipiga stori walivyozidi kunyamaza na hivyo kulala. Japokuwa Edson alilala
lakini Anita hakuthubutu hata kuyafumba macho yake.
Kichwa chake kilikuwa na mawazo tele juu ya mwanaume wa kwanza kuwa
naye katika uhusiano wa kimapenzi, Edson. Aliuhisi moyo wake kuwa kwenye
mapenzi na mwanaume huyo kwani hata kipindi cha nyuma walipokuwa wameachana,
hawakuachana kwa maneno wala ugomvi, waliachana kwa sababu tu masomo yaliwatenga.
Alitaka kupata nafasi ya kukaa naye na kuzungumza naye, alitaka
kufahamu mengi yaliyotokea, si maisha yale aliayopitia ambayo yalijaa shida,
bali alitaka kufahamu kama bado alikuwa akimpenda au la.
Alibaki kwenye kiti huku akijifikiria ni kwa namna gani angekwenda
kule alipokuwa Edson na kuzungumza naye, mume wake alikuwa pembeni yake ila
alikuwa amelala lakini hakuona kama ingekuwa rahisi kwake kumfuata na kupiga
naye stori.
Muda ulizidi kwenda mbele, akajua kwamba endapo boti ingefika
Zanzibar basi asingeweza kuzungumza na Edson, hivyo ilikuwa ni lazima aonane na
mwanaume huyo hata kabla boti haijafika Zanzibar na kuachana.
“Ni lazima nikazungumze na Edson, siwezi kusubiri hapa,” alisema
Anita.
Hakutaka kuendelea kusubiri, ilikuwa ni lazima akazungumze na
mwanaume huyo, hakuwa tayari kujiona akisubiri zaidi, alichokifanya ni kusimama
na kuanza kuelekea upande ambao ulikuwa na mizigo, sehemu ambayo ndipo Edson
alipokuwepo.
Wakati anapiga hatua kuelekea huko, ghafla akashtukia tumbo likianza
kuchafuka, akaanza kuyumba huku na kule na hapohapo kuanza kutapika. Hakuchukua
mifuko kama abiria wengine, hivyo matapishi yake yote yakaenda chini.
Mawimbi yaliendelea kupiga huku na kule, meli ile ikaanza
kuyumbishwa, kila mtu akaonekana kuogopa, bahari ilichafuka na hali ya hatari
kuonekana ndani ya meli hiyo.
Haikuwa kawaida, ni kweli wakati mwingine bahari huchafuka lakini
kwa siku hiyo ilikuwa zaidi. Boti ilipigwa na mawimbi mazito kiasi kwamba hata
wale abiria waliokuwa wamelala, wakaamka.
Phillip aliposhtuka kutoka
usingizini, mtu wa kwanza kabisa kumwangalia alikuwa mkewe, hakuwepo pale
alipotakiwa kuwepo, akajaribu kuangalia huku na kule lakini hakumuona, si yye
tu bali hata mtoto, naye hakuwepo.
Alichanganyikiwa, hakutaka kubaki mahali pale, tayari abiria
walianza kupiga kelele za kutaka kuokolewa kwani kwa jinsi hali ilivyoonekana
hakukuwa na dalili kwamba wangebaki salama kabisa.
Phillip akatoka nje ya sehemu aliyokuwa amekaa na kuanza kuangalia
huku na kule, alipoona kwamba mkewe hamuoni, akaanza kuita huku akionekana
kuchanganyikiwa.
“Anita...Anita...” aliita huku akiangalia huku na kule lakini
hakuweza kumuona mkewe.
Watu wakaanza kukimbia huku na kule kwa kuamini kwamba wangeweza
kuyaokoa maisha yao lakini hilo halikuwafanya kutoka nje ya meli, walibaki mule
mule.
Mawimbi mazito yaliendelea kuipiga boti ile, katika hali ya
kushangaza, maji yakaanza kuingia ndani ya boti ile hali ilizidi kumtia hofu
kila abiria.
“Tusaidieni tunakufaaaa...” alisema abiria mmoja.
Hali ikawa mbaya, mawingu mazito yakaanza kujikusanya angani na wala
hazikupita dakika nyingi, mvua ikaanza kunyesha. Ndani ya meli hakukukalika,
kila mmoja alikuwa akihangaika kuyaokoa maisha yake.
Anita pale alipokuwa alikuwa kwenye hali mbaya, alijitahidi kusimama
ili kurudi alipotoka lakini hakuweza, boti ilikuwa ikiyumbayumba sana kutokana
na kupigwa na mawimbi.
Maji yaliendelea kuingia ndani ya boti, nahodha na wafanyakazi
wengine walijitahidi kutafuta mawasiliano ya simu lakini hayakupatikana
kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.
Baada ya dakika kumi, boti ikaanza kuzama kutokana na maji mengi
kuingia ndani. Hakukuwa na maboya ya kutosha hivyo abiria wengi kuhofia
kufariki dunia ndani ya boti ile.
“Tunakufaaa...” walisema abiria katika kipindi ambacho boti
iliendelea kuzama.
Hakukuwa na mtu aliyemsaidia mwenzake, walikuwa katikati ya bahari,
katika kila upande, hakukuonekana kuwa na dalili za nchi kavu, hakukuwa na
aliyejua pande za dunia yaani Kusini ilikuwa wapi na Kaskazini ilikuwa wapi.
Boti ilizama, abiria wenye ujuzi wa kuogelea wakaanza kuogele kwa
staili ya kulegeza miili yao na kubaki juu wakielea, kwa wale ambao hawakuwa na
uwezo wowote ule, wakaanza kuzama na kufa huko baharini.
Wakati boti ikizama, Edson alikuwa katika chumba cha mizigo. Kwa
jinsi boti ile ilivyokuwa ikiyumbishwa, hali iliyokuwepo baharini alijua kwamba
kulikuwa na hatari ya boti kuzama humo baharini, alichokifanya ni kuelekea nje.
Huko, hapohapo akaanza kumtafuta Anita, alijua kwamba msichana huyo
hawezi kuogelea hivyo hakutaka kuona akifa, alimpenda kwa moyo mmoja, aliendelea
kumtafuta zaidi.
Mpaka boti inaanza kuzama, hakuwa amemuona Anita. Alijitahidi kuita
huku na kule, tena kwa sauti kubwa lakini hakusikia msichana huyo akiitikia,
moyo wake ulimuuma mno.
Kwa kuwa alikuwa na ujuzi wa kuogelea, akaanza kuogelea na kumtafuta
Anita. Kila alipopita, watu walikuwa wakilia na kuomba msaada. Hakutaka
kumsaidia mtu yeyote yule, kwa wakati huo, mawazo yake yalikuwa kwa Anita tu.
Alikuwa akimtafuta kwa kupiga mbizi huku na kule.
Ndani ya dakika tano nzima tangu boti izame, hakuweza kumuona Anita.
****
Maji yaliingia ndani ya boti na hivyo kuanza kuzama. Anita alipiga
kelele za kuomba msaada huku mkononi akiwa na mtoto wake lakini hakukuwa na mtu
aliyemsaidia, kila mmoja alikuwa bize kuyaokoa maisha yake lakini si kumsaidia
mtu mwingine.
Mbele yake alikiona kifo, hakuwa na uhakika kama angepona, kwake,
alijua kwamba ilikuwa ni lazima kufa, hivyo akaanza kusali sala yake ya mwisho
na kuyakabidhi maisha yake na ya mtoto wake mikononi mwa Mungu.
Boti ilipozama, hakukuwa na msaada wowote ule, alikuwa radhi kunywa
maji lakini si kuona maji yakimuua mtoto wake, hivyo alijitahidi kumshika kwa
mkono mmoja na kumpeleka juu huku miguu yake ikifanya kazi ya kukata maji ili
asizame.
Wakati akiwa kwenye harakati za kujiokoa yeye na kumuokoa mtoto
wake, akaanza kusikia akiitwa jina lake. Kitu cha kwanza akaisikiliza sauti ile
kwa makini, alichohisi ni kwamba alikuwa akiitwa na mumewe, Phillip lakini
alipoisikia vizuri sauti ile, haikuwa ya mumewe bali ilikuwa ni ya aliyekuwa
mpenzi wake, Edson.
“Anita…..Anita…Anita….” iliendelea kusikika sauti ya Edson.
“Edson…Edson nisaidie naku…” alisema Anita lakini hata kabla
hajamaliza sentensi yake akaanza kunywa maji.
Japokuwa kulikuwa na kelele mahali hapo lakini Edson aliweza
kuisikia sauti hiyo, alijua ilipotokea hivyo kuanza kupiga mbizi kuelekea kule
sauti ilipotokea.
Alipofika huko, akaanza kuangalia huku na kule, tayari watu wengine
walikuwa wamekufa, miili yao ilielea hivyo watu wengine kuishikilia miili hiyo
ili wasizame.
Edson alipomuona Anita, hapohapo akaanza kumsogela, alipomfikia,
kitu cha kwanza akamchukua Cynthia.
“Vipi Anita?” aliuliza Edson.
“Ninakufa Edson, ninakufaaaa.”
“Huwezi kufa! Hautoweza kufa. Kama utakufa, basi acha na mimi nife,” alisema Edson huku macho yake tu yakionekana kumaanisha alichokisema.
“Huwezi kufa! Hautoweza kufa. Kama utakufa, basi acha na mimi nife,” alisema Edson huku macho yake tu yakionekana kumaanisha alichokisema.
Alichokifanya, mkono mmoja ukamshikilia mtoto Cynthia aliyekuwa akilia
huku akipiga mbizi na kumwambia Anita amfuate kule alipokuwa akielekea. Safari
yao fupi iliishia sehemu iliyokuwa na pipa moja kubwa lililokuwa likielea na
kumwambia Anita alishikilie pipa hilo kwani ndiyo ulikuwa msaada pekee
waliokuwa nao.
Watu wengine waliendelea kufa, kelele zilianza kupungua kwani pamoja
na kuwa kwenye hali mbaya, mvua ile iliyokuwa ikiendelea kunyesha ikasababisha
baridi kali lililowamaliza watu wengi baharini hapo.
Alichokifanya Edson ni kumshikilia vizuri Cythia, akamwambia Anita
ajitahidi akae juu ya pipa lile kwani ndiyo ingekuwa nafasi pekee ya kuyaokoa
maisha yake.
Alichokifanya Anita ni kuanza kupanda pipa lile. Haikuwa kazi
nyepesi hata kidogo, alijitahidi sana kupanda, alitumia muda wa dakika kumi
nzima ndipo akafanikiwa na hivyo kuwa juu ya pipa lile kisha Edson kumpa
Cynthia.
“Na wewe panda!”
“Hapana Anita! Sitoweza kupanda.”
“Nashukuru kwa msaada wako Edson, nashukuru kwa kuokoa maisha
yangu,” alisema Anita huku akimwangalia Edson usoni.
“Usijali! Nimefanya hivi kwa kuwa ninakupenda sana Anita. Siku zote
nimekuwa nikikufikiria, sikujua ni kwa namna gani ningeweza kukuona tena,”
alisema Edson huku akimwangalia Anita.
Huo haukuwa mwisho, waliendelea kukaa baharini mpaka ilipofika jioni
ya saa kumi na mbili ndipo kwa mbali walipoona Boti ya Mv Space ikiwa
inakaribia kule walipokuwa.
Walikuwa kwenye hali mbaya, baridi liliwapiga na njaa ziliwauma mno.
Kuna kipindi walifikiria kwamba hata Cynthia alikufa kwani alikuwa kimya kabisa
hali iliyomfanya mara kwa mara Anita kumtingisha, alipoona akianza kulia,
alimuacha.
“Edson…Edson…boti,” alisema Anita kwa sauti ya chini, alikuwa
akimwamsha Edson aliyeonekana kuwa kwenye mawazo mengi.
“Unasemaje?” aliuliza Edson huku akitetemeka, nusu ya mwili wake
ilikuwa majini.
“Boti…”
Aliposikia neno boti akapata nguvu na kuona kwamba hiyo ndiyo
ilikuwa nafasi yao ya kuokolewa. Akatupia macho kule alipoambiwa kwamba
kulikuwa na boti, kweli aliiona ikiwa inasogea kule walipokuwa.
Alichokifanya ni kupunga mkono wake mmoja huku akipiga kelele za
kuomba msaada. Hiyo ilionekana kusaidia kwani watu waliokuwa kwenye boti ile
waliamua kuzungukazunguka katika eneo lile boti ilipozama ili kuona kama kuna
majeruhi basi wawasaidie kwani hali ilionekana kuwa mbaya.
“Tupo haiiiii….tupo haiiiiii….” alipiga kelele Edson.
Hiyo ilisaidia kwa kiasi kikubwa, watu wale waliokuwa kwenye boti
ile walipoisikia sauti ya Edson, wakaanza kuangalia kule sauti hiyo ilipotoka, kwa
bahati nzuri wakamuonaAnita akiwa juu ya pipa, kwa pembeni alikuwepo mwanaume
mwingine.
“Wale kule…” alisema mwanaume mmoja na hivyo kusogea kule kisha
kuwatupia boya lililofungwa kamba, walipolishika, wakaanza kuwavuta. Huo ndiyo
ukawa msaada kwao.
****
Taarifa zilitolewa katika vyombo vya habari hasa redio na
televisheni kwamba boti moja ya Royal Palm ambayo ilikuwa ikifanya safari zake
kwenda Unguja na Pemba ilipata ajali na abiria wengi kufariki.
Kila mtu aliyesikia taarifa hiyo, alisikitika, wengine hasa
waliokuwa na ndugu zao wakalia na kuomboleza kwa kujua kwamba wasingeweza
kuwaona tena ndugu wao hao.
Miili ya watu waliokufa katika ajali hiyo ikaokolewa na kupelekwa
hospitalini ambapo huko watu walitakiwa kwenda ili kuona kama kulikuwa na ndugu
zao hivyo kuichukua miili hiyo na taratibu nyingine kufuata.
Mtu ambaye alikuwa mmoja wa watu waliofika hospitali na kuiangalia
miili hiyo alikuwa Anita na baadhi ya ndugu zake. Alifika hapo kwa ajili ya
kuutafuta mwili wa mume wake aliyempenda, Phillip.
Walipelekwa katika chumba kilichokuwa na miili hiyo, walifunuliwa miili yote na kuonyeshewa, hakukuwa na mwili wa Phillip kitu kilichoonyesha kwamba mume wake huyo alikufa na mwili wake kuliwa na samaki.
Walipelekwa katika chumba kilichokuwa na miili hiyo, walifunuliwa miili yote na kuonyeshewa, hakukuwa na mwili wa Phillip kitu kilichoonyesha kwamba mume wake huyo alikufa na mwili wake kuliwa na samaki.
“Miili ndiyo hii tu?” aliuliza Anita huku akionekana
kuchanganyikiwa.
“Ndiyo hii tu! Hakuna mingine.”
“Kweli?”
“Ndiyo! Lakini subiri kwanza,” alisema daktari mmoja.
“Ndiyo! Lakini subiri kwanza,” alisema daktari mmoja.
Akaondoka na kuwaacha watu hao wakiwa katika mabenchi hospitalini
hapo wakilia tu. Anita alimuomba Mungu ili amfanikishe kumuona mume wake na
hata kama hatomuona basi angeridhika zaidi kama angeuona mwili wake tu.
Ndugu zake wakajaribu kumbembeleza lakini hakunyamaza, moyo wake
ulikuwa kwenye maumivu makali mno, hakutaka kusikia la mtu yeyote yule, kile
alichotaka kukisikia ni kuhusu mume wake tu.
Daktari yule aliporudi, wakasimama na kumsogelea, walitaka kusikia
kile kilichotokea kule alipokwenda kama aliweza kumuuona mwili wa Phillip au
la.
“Vipi?”
“Huko nilipokwenda wamesema kwamba miili ya wahanga wa ajali ya boti
ni hii tu,” alisema daktari yule.
Kilio zaidi kikaanza kusikika kutoka kwa Anita, hakuamini kama kweli
huo ndiyo ulikuwa mwisho wa kumuona mume wake mpendwa. Alibaki akiwa na maumivu
mazito moyoni mwake, huzuni aliyokuwa nayo haikuweza kusimulika.
Alilia na kulia lakini ukweli ulibaki palepale kwamba mwili wa mume
wake haukuwepo na kulikuwa na uwezekano kwamba ulilikuwa na samaki huko
baharini.
Kilichofuata baada ya hapo ni kuweka mazishi, watu wengi walikwenda
katika msiba huo mzito. Kilio cha Anita kilimhuzunisha kila mtu aliyekuwepo
mahali pale, alilia kwa kulalamika kwamba Mungu aliamua kumuonea kwani hata
mwili wake ungekuwa umepatikana, kwake ingekuwa faraja kubwa mno.
Baada ya saa kadhaa, jeneza likaletwa, padri akasimama na kuomba
sala maalumkisha safari ya kuelekea makaburini kuanza.
Ndani ya jeneza lile hakukuwa na mwili wake, kulikuwa na nguo zake
tu na baadhi ya vitu alivyokuwa navyo. Phillip alifariki kwa maana hiyo mali
zote alizokuwa nazo, ule utajiri mkubwa aliokuwa akiumiliki ulikuwa chini ya
mke wake ambaye alimuacha akiwa na mtoto wake mdogo, Cynthia.
“Pole sana Anita! Mungu atakupigania tu,” alisema mama yake, bi
Lydia.
“Nashukuru mama, asante kwa kunitia moyo katika kipindi hiki
kigumu,” alisema Anita.
*****
Kitu kilichokuwa kikimuumiza Anita ni kumuona mpenzi wake wa kipindi
cha nyuma, Edson akiwa kwenye hali ya umasikini mkubwa. Moyo wake uliumia mno,
hakuamini kama kulikuwa na mwanaume aliyekuwa akipata tabu kama alizokuwa
akipata Edson.
Moyo wake ulimpenda mno, mbali na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa
mwanaume huyo, pia alihitaji kuishi naye, yaani lile penzi la dhati alilokuwa
nalo lirudi na kuwa kama zamani.
Anita hakutaka kutulia, ni mwezi mmoja tu ndiyo ulikuwa umepita
tangu mazishi ya mumewe yalipofanyika lakini hakutaka kutulia, kila siku akawa
mtu wa kumpigia simu Edson na kuzungumza naye, alishindwa kuzizuia hisia za
kimapenzi alizokuwa nazo juu yake hivyo kumwambia ukweli.
Edson hakutaka kupinga, alijua hilo lingetokea na yeye mwenyewe
alimpenda mno mwanamke huyo, hivyo kuanza kwenda kwake na kufanya mambo mengine
kama wapenzi.
Kwenye kitanda kilekile alichokuwa akikitumia na mumewe ndicho
hichohicho alicholala na Edson, hakutaka kujali sana kuhusu Phillip kwani kama
kufa alikwishakufa hivyo asingeweza kurudi tena duniani.
Uhusiano huo uliendelea kwenda mbele, waliendelea kupendana kama zamani.
Ndugu wa Phillip waliposikia kwamba Anita aliamua kuwa na mwanaume mwingine,
mioyo yao iliumia sana, hawakuamini kwamba Anita hakusubiri hata miezi sita
iishe, aliamua kuwa na mwanaume mwingine kwa haraka sana.
“Jamani! Nasikia Anita amepata mwanaume mwingine!” alisema ndugu
mmoja huku akionekana kushangaa mno.
“Hata mimi mwenyewe Joshua aliniambia hivyohivyo, bado sijapata
uhakika, hebu nikamuulize Joyce, anaweza akawa anajua,” alisema msichana mwingine.
“Lakini mbona amefanya haraka sana?”
“Hata mimi sijui kwa nini, unajua ni miezi miwili tu imepita.”
“Ndiyo hivyo! Ninachojiuliza, ni kwa muda gani alikutana na mwanaume huyo, kuzungumzia mapenzi mpaka kuwa wapenzi, ni muda mchache sana, yaani sijui nini kilitokea,” alisema msichana huyo.
“Ndiyo hivyo! Ninachojiuliza, ni kwa muda gani alikutana na mwanaume huyo, kuzungumzia mapenzi mpaka kuwa wapenzi, ni muda mchache sana, yaani sijui nini kilitokea,” alisema msichana huyo.
Kila mmoja alishangaa, kila walichojiuliza, hawakupata jibu lolote
lile. Mioyoni mwao waliumia lakini hawakuwa na jinsi, Anita aliamua kuwa na
mwanaume mwingine hivyo hakutaka kuingiliwa.
Baba yake Edson aliposikia hivyo, hakutaka kukubali hata kidogo,
alichokuwa akikiangalia ni mjukuu wake, Cynthia tu, alichokifanya ni
kuwasiliana na Anita, majibu aliyopewa ni kwamba asiingiliwe, alichokiamua
kilikuwa ni matakwa yake, hivyo hakutaka kuingiliwa.
“Unasemaje?”
“Ndivyo alivyoniambia! Tusimuingilie,” alisema baba Edson.
“Anita hawezi kubadilika namna hiyo! Kweli?”
“Ndiyo!”
“Hapana!”
“Hapana!”
“Kwani kwenye simu hujasikia mke wangu? Amenijibu tena kwa nyodo.”
“Yaani Anita huyuhuyu?”
“Ndiyo!”
“Ndiyo!”
Alichokifanya baba Edson ni kuwasiliana na wazazi wa Anita ambao
wakamuita binti yao na kumwambia kwamba hakutakiwa kuwa na uhusiano na mwanaume
yeyote yule mpaka kipindi cha miezi sita kipite.
MAjibu waliyopewa na binti yao, hayakuwa mazuri, bado msichana huyo
hakutaka kuingiliwa katika maisha yake. Wazazi wake walihuzunishwa na majibu ya
binti yao, walijaribu kumuomba kwamba auondoe moyo wake kwa Edson lakini
msichana huyo hakukubali, kwa wakati huo, hakukuwa na mwanaume aliyeuteka moyo
wake zaidi ya Edson.
“Tunataka uachane naye, mlee mwanao kwanza,” alisema baba yake.
“Jamani mbona tunaingiliana? Baba, ulivyoanza uhusiano na mama kuna
mtu aliwaingilia?” alihoji Anita.
“Anita…maneno gani hayo?”
“Nimeuliza tu! Kama hakuna aliyewaingilia, kwa nini nyie
mnaniingilia mimi?” aliuliza Anita.
Anita alibadilika, alionekana kuwa jeuri, hakutaka kusikia kitu
chochote kile kutoka kwa mtu yeyote, alichokiangalia kwa wakati huo ni kuwa na
Edson tu. Alimpenda zaidi ya mtu yeyote, katika maisha yake, hakukuwa na mtu
ambaye angeweza kumtenganisha na Edson.
Miezi ikakatika, mwaka mwingine ukaingia, Cynthia akatimiza miaka
mitatu hivyo kuanza kusoma shule ya chekechea katika Shule ya Kimataifa ya St.
Augustine, shule iliyokusanya watoto wengi wa watu wenye hela.
Japokuwa maisha yalikuwa ya kifahari, alipata alichokitaka lakini
Edson hakuonekana kuwa na furaha, kila siku alionekana kuwa na mawazo mengi,
alionekana kama mgonjwa hali iliyomuweka Anita kwenye wakati mgumu.
Hakupenda kumuona mwanaume wake akiwa hivyo, kitendo cha kuonekana
mnyonge hata yeye mwenyewe kilimshangaza mno. Aliumia moyoni, alijua kwamba
kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea ila Edson alifanya kuwa siri kubwa.
Kuvumilia kwake kukaisha, hakutaka kuendelea kujiuliza maswali mengi
juu ya kilichomsibu Edson, alichokifanya Anita ni kumuita na kumuuliza kile
kilichokuwa kikiendelea ambacho kilimfanya kuwa kwenye hali ile.
“Tatizo nini mpenzi?” aliuliza Anita.
“Hivi unanipenda kweli?” aliuliza Edson.
“Ndiyo! Ninakupenda mpenzi.”
“Kweli?”
“Hakika! Hakuna mwingine zaidi yako!”
“Kweli?”
“Hakika! Hakuna mwingine zaidi yako!”
“Haiwezekani! Sidhani kama ni kweli!”
“Kweli mpenzi! Ninakupenda. Unataka nikufanyie nini mpaka ujue
kwamba ninakupenda?” aliuliza Anita.
Edson hakuzungumza kitu, akabaki kimya huku akiwa amejiinamia. Bado
alijifanya kuwa na mawazo mengi, Anita alibaki akimwangalia huku akihisi moyo
wake kuumia mno. Alichokifanya ni kumsogelea na kumuinua, alipomwangalia Edson,
machozi yalikuwa yakimtoka mwanaume huyo.
“Unalia nini tena mpenzi?” aliuliza Anita.
“Kwa sababu haunipendi!”
“Ninakupenda mpenzi! Ninakupenda na ndiyo maana upo hapa!”
“Hapana Anita! Sidhani kama ni kweli!”
“Edson! Niambie mpenzi nikufanyie nini!”
“Mimi ni nani kwako?”
“Mpenzi wangu!”
“Mpenzi wangu!”
“Na umesema kwamba muda si mrefu tutaoana, si ndiyo?”
“Ndiyo mpenzi!”
“Ndiyo mpenzi!”
“Sasa mbona kila kitu unajimilikishia wewe tu?”
“Sijakuelewa.”
“Namaanisha mali. Yaani kila kitu unataka uonekane wewe tu.”
“Yaani bado sijakuelewa.”
“Sijakuelewa.”
“Namaanisha mali. Yaani kila kitu unataka uonekane wewe tu.”
“Yaani bado sijakuelewa.”
“Namaanisha mbona na mimi hutaki kunipa haki yangu!”
“Ipi?”
“Ya kumiliki!”
“Ipi?”
“Ya kumiliki!”
“Hizi mali?”
“Ndiyo!”
“Sasa hilo ndiyo linakufanya uhuzunike hivyo?”
“Ndiyo!”
“Sasa hilo ndiyo linakufanya uhuzunike hivyo?”
“Sasa unafikiri nitakuwa na furaha? Naendesha magari ya kifahari,
ila sina haki nayo, naishi kwenye nyumba nzuri, ila sina haki nayo, nasimamia
mpaka biashara ambazo sina haki nazo. Sasa haki zangu zipo wapi?” alihoji
Edson.
“Sasa ndiyo ukasirike na kuonekana kama mgonjwa?”
“Ndiyo hivyo!’
“Basi usijali mpenzi, nitakuandikisha na wewe uwe na haki nazo,”
alisema Anita maneno yaliyomfanya Edson kuwa na furaha mno.
Hilo ndilo alilolitaka, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali kila
alipojiona akiendesha magari ambayo si yake au kuishi ndani ya nyumba ambayo
haikuwa na haki yake. Kila siku katika maisha yake alitamani naye awe na
asilimia fulani katika kumiliki mali zile alizokuwa nazo Anita.
Kutokana na mapenzi mazito aliyokuwa nayo Anita kwa Edson, akajikuta
akimuita mwanasheria wake na hatimaye kumuandikisha Edson kuwa mmiliki halali
kama alivyokuwa.
Kwa Edson, hiyo ilikuwa furaha kubwa, hakuamini kama kila kitu
kingekwenda kwa wepesi kama kilivyokuwa. Akajikuta akimkumbatia Anita na
kummwagia mabusu mfululizo, hapo, akamwambia kwamba moyoni mwake alikuwa na
amani, furaha aliyokuwa nayo haikuelezeka.
Anita alimpenda sana Edson lakini mwanaume huyo, moyoni mwake
alikuwa akifikiria kitu kingine kabisa, hakujiona kama alikuwa na mapenzi
makubwa kwa msichana huyo kama kipindi cha nyuma, kitu ambacho kilimfanya
kujifanya kuwa na mapenzi mazito kwa msichana huyo ni mali alizokuwa nazo tu.
Alizitamani mali zile, alitaka sana ziwe zake, hivyo kitendo cha
kuandikishwa kama mmiliki halali wa zile mali, moyoni mwake ilikuwa ni shangwe
kubwa.
Akapanga mipango yake, kitu pekee alichotaka kufanya ni dhuluma tu,
alitaka kumdhulumu mwanamke huyo mali zile, ziwe zake na kufanya mambo yake,
azitumie atakavyo.
“Ameingia kingi! Ataisoma namba sasa,” alisema Edson huku meno yote
yakiwa nje.
****
Siku zikaendelea kukatika, baada ya miaka miwili kupita huku Cynthia
akiwa na miaka mitano, hapo ndipo Edson alipoanza kubadilika. Akaanza dharau
kwa Anita, kila alipoambiwa hili na lile, alibadilika na hakutaka kusikia hata
mara moja.
Akawa mtu wa kunywa pombe, kurudi usiku wa manane na hata wakati
mwingine kuwaingiza wanawake ndani ya nyumba hiyo kitu kilichomuuma sana Anita.
Hakuwa na msemo wowote ule. Kwa kipindi kirefu alimwambia kwamba
ilikuwa ni lazima waoane lakini kwa kipindi hicho, Edson hakutaka kusikia
chochote kile, hakutaka kusikia mambo ya ndoa kwani kile alichokitaka
alikifanikisha kwa kiasi kikubwa.
Alitaka kila kitu kiwe chake, hivyo akaanza kuhamisha fedha
zilizokuwa kwenye akaunti za Anita na kuziingiza katika akaunti yake. Kiasi cha
shilingi bilioni sitini kikaamishwa na kuingizwa katika akaunti yake.
Anita hakufahamu kilichokuwa kikiendelea, kila kitu alichangia na
Edson, hakujua kama mule ndani ya akaunti yake ni milioni kumi tu ndizo
zilizokuwa zimebaki.
Maisha yalibadilika, hayakuwa yale yenye mapenzi kama yalivyokuwa
kipindi cha nyuma, Edson yule alibadilika, Anita hakuamini kama mwanaume
yuleyule aliyemkuta akiwa amechoka katika kampuni moja ya boti za Royal Palm
ndiye ambaye leo hii alikuwa akimfanyia mambo yale.
Moyoni aliumia, wakati mwingine alijuta sababu ya kumwandika kama
mmoja wa wamiliki wa mali zile.
Hapo ndipo tabia halisi ya Edson ilipoanza kuonekana, ulevi
ukamteka, mara kwa mara akawa mtu wa kurudi usiku wa manane. Kila Edson
anapokuwa nje, Anita hakulala, alibaki macho huku akimsubiria mwanaume huyo.
Mateso aliyoyapata yalikuwa siri, hakutaka kumwambia mtu yeyote kwa
kuogopa kuchekwa na kudharauliwa. Alikuwa mtu wa kujifungia chumbani, wakati
mwingine alibaki akilia tu, kila kilichokuwa kikiendelea, hakika kilimuumiza
mno.
“Edson…mbona umebadilika hivi?” aliuliza Anita.
“Nani? Mimi?”
“Ndiyo! Haukuwa hivi zamani, nini kimekubadilisha?” aliuliza Anita,
machozi yalianza kumlenga.
“Hebu niondolee uchuro wako huko,” alisema Edson huku chupa ya Saint
Anna ikiwa mkononi mwake.
Kubadilika kwa Edson kuliendelea kumshangaza sana Anita, hakutaka
kukubali, alijua kulikuwa na kitu kilichomfanya kuwa hivyo, akili yake
ikamwambia kwamba ilikuwa ni lazima afuatilie suala la fedha katika akaunti
zake kwa kuhisi kwamba Edson angeweza kumtapeli.
Hapo ndipo alipoanza kufuatilia, alipokwenda kwenye akaunti ya
kwanza, hakukuta kiasi cha fedha kikubwa, ni milioni tano tu ndizo zilizokuwa
zimebaki.
Alishtuka mno, hakuamini macho yake, hakutaka kuishia hapo,
alipoangalia akaunti ya pili, pia kulikuwa na shilingi milioni tano tu.
Alijikuta miguu yake ikiisha nguvu, ikalegea na hapohapo kuanza kulia kama mtoto.
“Kuna nini dada?” aliuliza mfanyakazi wa benki, si yeye
aliyeshangazwa na kilio cha Anita, hata wafanyakazi wengine na wateja waliokuwa
humo ndani walishangazwa naye.
Watu wakaanza kumbembeleza Anita, walimtaka anyamaze lakini pia
walitaka kufahamu tatizo lilikuwa nini. Anita hakunyamaza, kilichokuwa
kimetokea, wakati mwingine alihisi kama yupo ndotoni na baada ya muda mchache
angeamka kutoka usingizini.
Anita hakutaka kubaki hapo benki, alichokifanya ni kuondoka huku
akiwa amechanganyikiwa, alipofika nje, akalifuata gari lake la thamani na
kuingia, safari iliyoanza ni kwenda nyumbani kwake.
Aliendesha gari huku akiwa amechanganyikiwa, kila aliposogea mbele, alisikia
maumivu mazito moyoni mwake. Hakuamini kama Edson yuleyule ndiye aliyefanya
vile, hakuamini kama shukrani ya punda aliamua kumpiga mateke.
Kwa kuwa hakukuwa na foleni, hakuchukua muda mrefu akawa
amekwishafika nyumbani, geti likafunguliwa na kuingia ndani.
“Hili gari la nani?” aliuliza Anita mara baada ya kuingia ndani ya
eneo la nyumba yake.
“Kuna wageni wamekuja.”
“Wakina nani?”
“Wakina nani?”
“Sijui! Ila shemeji amesema ni wateja wamekuja kununua nyumba.”
“Nyumba ipi?”
“Hiihii!”
Anita alihisi kuchanganyikiwa zaidi, hakuamini kile alichokisikia
kwamba kuna wageni wamekuja kwa lengo la kununua nyumba. Akaingia ndani mpaka
sebuleni, macho yake yakagongana na wanaume wawili waliovalia suti ambao
walikaa kwa kujiachia sebuleni pale.
Mbali na wanaume hao, pia Edson alikuwa sebuleni hapo akiwa
amejiachia tu, uso wake ulikuwa kwenye tabasamu pana.
“Milioni mia moja na hamsini,” alisema Edson, alijifanya kama
kutokumuona Anita.
“Basi hakuna tatizo! Hati iko wapi?”
“Hilo halina tatizo!”
“Sawa! Kesho nitakuandikia cheki,” alisema mwanaume mmoja, alikuwa
kijana tu.
Anita hakuamini alichokisikia, mapigo ya moyo wake yalidunda kwa
nguvu, hakuamini kile alichokiona, hakuamini kama hao waliofika nyumbani hapo
walikuwa wateja waliotaka kununua nyumba pasipo yeye kushirikishwa.
Moyo wake ulikuwa na hasira mno, alitoka benki ambapo huko alikuta
kiasi kikubwa cha fedha kikiwa kimechukuliwa, wakati akirudi nyumbani huku
akionekana kuwa na hasira, akakutana na kitu kingine kabisa, wageni walifika
mahali hapo kwa ajili ya kununua nyumba yake.
“Edson! Unataka kuiuza nyumba yangu?” aliuliza Anita huku akionekana
kutokuamini.
“Kuuza nyumba yako au yetu?”
“Yetu! Tangu lini? Umechangia hata tofali humu?” aliuliza Anita,
hakuamini kama siku hiyo alimfokea Edson.
“Kwani hati ya nyumba inaonyesha ni nani mmiliki halali wa nyumba
hii?”
“Mimi?”
“Umenisahau hata mimi? Sikiliza Anita, mimi kama mmoja wa wamiliki wa nyumba hii, nimeamua kuiuza kwa kuwa nimechoka kuishi humu, ni bora nyumba iuzwe, tugawane pesa halafu kila mtu afanye yake,” alisema Edson.
“Mimi?”
“Umenisahau hata mimi? Sikiliza Anita, mimi kama mmoja wa wamiliki wa nyumba hii, nimeamua kuiuza kwa kuwa nimechoka kuishi humu, ni bora nyumba iuzwe, tugawane pesa halafu kila mtu afanye yake,” alisema Edson.
Anita alibaki akibubujikwa na machozi tu, hakuamini kama kile
kilichokuwa kikitokea. Aliachiwa mali na mumewe, aliachiwa fedha nyingi lakini
mwisho wa siku, kila kitu kilikuwa kikiporwa na mwanaume aliyeonekana kuwa
katili.
Hakuacha kulia, aliumia mno lakini machozi yake yote, hasira zake
zote hazikuweza kubadilisha kitu chochote kile, ukweli ulibaki palepale kwamba
nyumba ilitakiwa kuuzwa na kisha agawane hela na Edson, mtu ambaye hakuwahi hata
kutokwa jasho kuzitafuta.
Baada ya wiki moja, uuzaji wa nyumba ile ukakamilika, haikuwa mali
yake tena, ilikuwa mali ya mtu mwingine, mmiliki mpya aliyejulikana kwa jina la
Andrew Nkone.
Hilo lilikuwa pigo kubwa kwa Anita, bado hakuamini kilichokuwa
kimetokea kwamba alipoteza nyumba na kiasi kikubwa cha fedha. Hakukuwa na
sehemu ya kukimbilia, kila alipokwenda, hakupata msaada wowote ule mpaka pale
alipoashauriwa kwamba ilikuwa ni lazima kesi hiyo ifikishwe mahakamani ili
aweze kushinda haki yake.
“Itawezekana kweli?”
“Kwa nini isiwezekane?”
“Naona inaweza kuwa na ugumu.”
“Hakuna kitu kama hicho! Wewe nenda tu.”
“Hakuna kitu kama hicho! Wewe nenda tu.”
Alichokifanya ni kuonana na mwanasheria wake na kumwambia kile
kilichokuwa kikiendelea hivyo kesi kufunguliwa na kuanza kusikilizwa
mahakamani.
“Hii ni kesi ya madai, nina uhakika utafanikiwa tu, utashinda na
kila kitu kurudi kwako,” alisema mwanasheria wake aitwaye Sifaeli Mambo.
“Nitashukuru sana, naomba unisaidie.”
“Hilo wala usijali.”
“Hilo wala usijali.”
Kilichotokea ni Edson kuitwa mahakamani na kusomewa kesi ya madai iliyokuwa
imepelekwa katika mahakama hiyo huku mshtaki akiwa Anita. Edson hakuonekana
kuwa na wasiwasi wowote ule, kila kitu kilichokuwa kimetokea, alikuwa na
uhakika kwamba angeshinda kesi ile na hivyo kujimilikisha haki za umilikaji wa
mali na fedha zile moja kwa moja.
Wakati kesi ikiunguruma mahakamani, hakukuwa na ndugu yeyote wa
Anita au marehemu mume wake aliyekwenda mahakamani, walitokea kumchukia Anita
kutokana na kile alichokuwa amekifanya hivyo nao walimwachia afuatilie kila
kitu peke yake.
Mtu ambaye alikuwa tumaini lake kwa wakati huo alikuwa mtoto wake tu
ambaye katika kipindi hicho alikuwa na miaka sita. Kila siku Cynthia alionekana
kuwa na huzuni mno, kila alipomuona mama yake akilia, moyo wake ulimuuma sana,
hakujua mama yake alilia nini, alijitahidi kuuliza lakini Anita hakutaka kumwambia
ukweli, alimficha.
Tofauti na kesi nyingine, kesi hiyo ilisikilizwa kwa muda wa miezi
miwili tu tena huku ikisimamiwa na hakimu aliyejulikana kwa jina la James
Marimba. Hukumu ya kesi ile ilivyotoka ilionyesha kwamba Anita alipoteza haki
zake za kumiliki mali zote, si hizo tu na hata fedha ambazo alitakiwa
kuzimiliki, hakuwa na haki nazo.
Kilisikika kilio kikubwa mahakamani hapo, hakuamini kama hakimu
ndiye aliyetoa hukumu hiyo nzito. Alipoteza kila kitu, alimpenda Edson,
alimthamini na kumpa kila kitu alichokihitaji kikiwepo uhalali wa kumiliki mali
lakini mwisho wa siku ni maumivu makali ndiyo yaliyofuata.
Itaendelea kesho
Post a Comment