Dallas wa Wolper afunga ndoa na Suleiya!

Jacqueline Wolper.
ALIYEKUWA
mchumba wa staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper, Ramadhan Mtoro
‘Dallas’ inadaiwa kuwa hivi karibuni amefunga ndoa na mwanamke mmoja
aliyefahamika kwa jina la Suleiya.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita maeneo
ya Mbezi-Ununio jijini Dar ambapo wawili hao walionekana wakiwa katika
hali ya furaha muda wote huku ndoa hiyo ikifungwa bila kificho.
“Hatimaye
leo yamekuwa, yaani yule jamaa (Dallas) aliyekuwa akimpatia Wolper
magari ya kifahari na mipesa leo hii saa saba mchana (Jumapili) anafunga
ndoa tena na mwanamke mwingine mkali kuliko hata huyo Wolper,” kilisema
chanzo.
Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Amani lilifanikiwa
kutimba eneo la tukio na kushuhudia Dallas akifunga ndoa kweli na
mwanamke huyo ambapo baadaye waliingia moja kwa moja kwenye gari na
kutokomea.
Miaka
mitatu iliyopita Dallas alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Wolper
hadi kufikia hatua bi’dada huyo kubadili dini ili aolewe naye lakini
mwishowe uhusiano huo uliyeyuka.
Post a Comment