CUF Yatangaza Maandamano Makubwa Dar es Salaam
Wanawake wa chama cha wananchi CUF maarufu kama JUKECUF wametangaza kufanya maandamano ya Amani siku ya tarehe 22,mwezi huu wa pili Jijini Dar es salaam yenye adhma ya kupinga hali ya kisiasa inayoendelea visiwani Zanzibar.
Akizungumza
na wanahabari mapema leo mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mh severena
mwijage amewaambia wanahabari kuwa maandamano hayo yataanzia ofisi kuu
za CUF buguruni kuelekea ofisi ya makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania Mh Samia Suluhu
Amesema
kuwa jumuiya hiyo inatambua kwamba hali ya Amani iliyopo Zanzibar
ikivurugika kwa kiasi kikubwa watakaoathirika ni kina mama na watoto
hivyo wameona ni bora kufikisha kilo chao hicho kwa makamu wa Rais
ambaye ni Mwanamke mwenzao awasaidie.
Maandamano
hayo yatapita barabara ya uhuru,ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es
salaam,karume,kariakoo,mnazi mmoja,Central polisi,barabara ya sokoine
,Bandarini,mahakama kuu,mahakama ya ardhi,Hadi ofisi ya makamu wa Rais.


Post a Comment