Simon Msuva wakishangilia na Paul Nonga moja ya magoli ya leo dhidi ya Friends Rangers
Yanga imefanikiwa kutinga raundi ya 16 bora ya michuano ya Azam
Sports Federation Cup kufuatia ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Friends
Rangers inayoshiiki ligi daraja kwanza. Mchezo huo umechezwa leo January
24 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Niyonzima leo alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Rangers mchezo wa FC Cup
Simon Msuva amefunga magoli mawili kwenye mchezo huo. Goli la kwanza
amelifunga dakika ya sita akiunganisha kwa kichwa krosi ya Issoufour
Bubacar kabla ya kuzama tena wavuni kupachika bao la pili kwa shuti kali
dakika ya 24 akiitendea haki pasi ya Paul Nonga ambaye leo amepoteza
nafasi lukuki za kufunga kwenye game hiyo. Paul Nonga leo ameshindwa kupachika mabao kutokana na nafasi alizopata
Matheo Anthony alikamilisha ushindi wa Yanga kwa kufunga bao la tatu
dakika ya 51 baada ya kuiweka kambani krosi ya Salum Telela.
Friends Rangers walijitahidi kucheza vizuri lakini walizidiwa mbinu
na uzoefu na wachezaji wa Yanga kwenye mchezo wa leo. Rangers
walitengeneza nafasi kadhaa lakini safu ya ushambuliaji iliyokuwa
ikiongozwa na Good Hamis akishirikiana na Eleciter Mpepo haikufua dafu
mbele ya ukuta wa Yanga uliotengenezwa na Vicent Bossou pamoja na Pato
Ngonyani.
Yanga wanaungana na Simba, Toto Africans, Ndanda FC, ambao walishinda
kwenye mechi zao za jana wakati Friends Rangers wao wameaga rasmi
mashindano hayo kwa msimu huu.
Post a Comment