TASWIRA YA SAMATTA ALIVYOMUONYESHA KIKWETE TUZO YAKE, NAYE AKAMKABIDHI JEZI YA TP MAZEMBE
Mshambuliaji nyota wa TP Mazembe na Taifa Stars, Mbwana Samatta leo amemkabidhi jezi yake Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.
Samatta
alikwenda kumtembelea Kikwete katika makao makuu ya CCM ambayo yeye ni
mwenyekiti wake na kumshukuru kutokana na mchango wake wakati akiwa Rais
wa Tanzania.
Baada
ya kumuonyesha tuzo yake ya Mwanasoka Bora Afrika ndani ya Afrika,
Samatta alimkabidhi Kikwete jezi namba 9 anayoivaa Mazembe. Alifanya
hivyo mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye.
Post a Comment