Ostaz Juma: Miaka 10 na wanamuziki ilitaka kunivunjia ndoa

Meneja wa muziki hapa Bongo, Ostaz Juma Namusoma.
Musa mateja
UKIANZA
kutaja majina ya mameneja mbalimbali wa muziki hapa Bongo, baadhi ya
majina makubwa yasiyoisha miongoni mwao huwezi kulikosa jina la Ostaz
Juma Namusoma.
Kwa mujibu wa kinywa chake mwenyewe Ostaz Juma Namusoma, juzikati
nilipata nafasi ya kumbana na kunieleza kiunagaubaga namna alivyoweza
kujipenyeza hadi kupata jina kupitia muziki wa Bongo.
Kwa
kinywa chake aliniambia kwamba, muziki kwake ni sehemu ya maisha ambayo
ameishi kwa kipindi kirefu sana, kwani tangu alipokuwa mdogo alipenda
muziki kushinda kitu chochote, msikie mwenyewe.
OSTAZ
JUMA: Mimi ni miongoni mwa vijana wa kipindi hicho ninayetokea Musoma
mkoani Mara. Nilianza kupenda muziki tangu nasoma shule ya msingi tena
mapema kabisa nikiwa darasa la tatu.
Nikiwa
shuleni nilikuwa napenda sana kuimba nyimbo mbalimbali za wasanii wa
Kongo hadi nikafikia hatua ya kununua redio na kuwarekodi watoto
wenzangu wakiimba kisha nazitunza nyimbo walizokuwa wakishindana kuimba
hasa za Boringo za Wazaire.

Nimefanya
hivyo hadi nikawa nagombezwa na wazazi wangu lakini sikukoma hadi
nilipokuwa mtu mzima na kuanza kujifanyia mambo yangu ambapo wazazi
hawakuweza kuniingilia.
Kwa
jinsi hii ndiyo utaweza kugundua kuwa nina kipaji cha kusimamia watu
ndiyo maana nimeweza kuwasaidia wanamuziki wengi tu kwenye dansi ambapo
kabla ya kujiingiza katika Bongo Fleva niliwahi kuwasaidia wanamuziki wa
dansi kama Ally Chocky, Super Nyamwela, Jose Mara, Kalala Junior,
Nyoshi El-Saadat, Mwinjuma Muumini na Mulemule.
Tabia
za wanamuziki kiukweli hazipishani sana hivyo ukiona meneja yeyote
analalamika juu ya wanamuziki basi ujue matatizo yao mara kadhaa
yamekuwa hayapishani sana, ila wanaopishana tabia na namna ya kuongoza
ni mameneja tu.

Namna
ya kuongoza na kummeneji mtu kunategemeana na uwezo wa kifedha na akili
pia, nasema hivyo kwa sababu muziki wetu umekuwa ukiyumba mara kadhaa
kutokana na baadhi ya mameneja kuwa wasimamizi wabovu na wengine
wanasimamia wakiwa hawana fedha ya kuweza kuwaongoza wasanii.
Meneja
ninayeweza kumpa saluti hapa Bongo ni Saidi Fella kwani ameonesha njia
kubwa ya kuimarisha Muziki wa Dansi na sasa umeanza kuwa juu kiasi cha
watu kuanza kuupenda tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ulianza
kupoteza dira.
ALIANZAJE KUSIMAMIA BONGO FLEVA?
Ostaz
Juma: Kwenye Bongo Fleva niliingia baada ya kuanza kumsimamia shemeji
yangu aitwaye Abdallah David aliyekuwa akijiita Fil David, huyu
nilijikuta namsimamia baada ya kumuona ana kipaji kizuri na baadaye
nikaanzisha rasmi kampuni yangu ya Mtanashati.
Mtanashati
ilipoanza tu nikapunguza kuwasaidia wanamuziki wa dansi hivyo
nikajikita kwenye Bongo Fleva ambapo nilianza kumsimamia marehemu Sharo
Milionea aliyemleta Kitale, lakini kabla sijaingia mkataba na Sharo
akafariki dunia.
Baada
ya kufariki kwa Sharo Milionea ambaye ndiye msanii naweza kujisifia
katika upande wa Bongo Fleva kwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana,
nilimchukua PNC, Dogo Janja na Happy Balis ambao nilifanyanao project
kibao kiasi ilifikia hatua nikawa nakosana hadi na mke wangu kisa muziki
huu.
Nimekuwa
nikiwasaidia wasanii hawa kwa muda lakini nilichoweza kujifunza ni
kwamba wasanii wengi hawana adabu kabisa, kwani kuna siku niliwahi
kukosana na mke wangu kwa kushindwa kumpeleka hospitali kisa kumpeleka
Dogo Janja kwenye interview jambo ambalo mke wangu amekuwa akinikumbusha
kila mara nami huwa halitoki kichwani hadi leo.
Fedha
niliyowahi kutumia hadi leo kwa ajili ya Dogo Janja na PNC naweza
kujenga hata ghorofa tatu hapa mjini, lakini kwa kuwa nilikuwa naupenda
muziki ndiyo maana leo utaona inafikia muda sasa nimeamua kuachana na
hawa Bongo Fleva maana hawana nidhamu hata tone ila ukilinganisha na
wanamuziki wa dansi utagundua ni bora dansi kuliko Bongo Fleva.
Nasema
wanamuziki wa dansi ni bora kuliko wa Bongo Fleva kwa sababu wakati
nadili na wanamuziki wa dansi walikuwa wanaonesha nidhamu ya hali ya juu
jambo ambalo wanalifanya hadi sasa.
Ujue
nilikuwa nikiwapatia fedha za kodi za nyumba, mara nyingine kama
Christian Bella na Chocky hawa niliwahi hata kuwalipia studio mara
kadhaa kwa ajili ya kurekodi nyimbo zao binafsi.
Christian
Bella yeye aliwahi hadi kunitungia wimbo ambao unaitwa Ubinadamu ambao
hata yeye ukimuuliza leo anaujua na ninao mimi mwenyewe.
Wasanii
wakijua kuwa muziki ni kazi na sehemu ya maisha yao basi hakuna Bongo
Fleva atakuja kushindwa kufanya mambo makubwa kama anavyofanya Diamond
kwani kinachomfanya kuheshimika na kufanikiwa ni nidhamu yake tu.
Post a Comment