Ofisi ya Kamishna Mkuu TRA Yavunjwa, Kompyuta Mbili Zaibiwa
Watu wasiojulikana wamevamia na kuvunja ofisi ya kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuiba kompyuta na vifaa vingine.
Habari
tulizozipata ambazo zimethibitishwa na Polisi kanda maalumu ya Dar
es Salaam zinasema miongoni mwa kompyuta zilizoibiwa ni ile
iliyokuwa inatumiwa na Dr Philip Mpango alipokaimu nafasi ya
Kamishna mkuu wa TRA kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha
Kwa
mujibu wa chanzo hicho,huenda kompyuta hiyo ikawa na taarifa muhimu
kuhusu ukwepaji wa kodi na sakata la makontena Bandarini.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu Ya Dar es salaam,Simon Sirro amesema tayari
jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa uchunguzi zaidi
Siro alitaja vitu vilivyoibwa katika ofisi hiyo kuwa ni Kompyuta mbili, Televisheni moja na King'amuzi.
Alisema
wanaoshikiliwa ni walinzi wawili kutoka kampuni ya Suma JKT
ambao walikuwa zamu usiku huo, Katibu Muhtasi pamoja na Karani
wa Ofisi hiyo.
Hata
hivyo, Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, amekanusha kutokea
kwa tukio hilo akisisitiza lilikuwa ni jaribio la wezi kutaka
kuvunja ofisi hiyo.
Kayombo
alisema hakuna wizi wowote uliotokea katika jaribio hilo kwa
sababu hawakufanikiwa kuingia ndani.Alisema mali zote ziko salama
na suala hilo limeripotiwa polisi kwa uchunguzi zaidi.

Post a Comment