ad

ad

Masogange adaiwa kutumia tunguri kujiongezea mvuto kunasa vigogo!


Ulozi? Video Queen wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ anadaiwa kutumia ‘tunguri’ kujiongezea mvuto ili kuwanasa vigogo.

Habari kutoka kwa chanzo kilicho karibu na Masogange zilieleza kwamba kuna waganga wawili wanaompa jeuri mrembo huyo, mmoja akiwa anaishi maeneo ya Mwenge, Dar na mwingine Bagamoyo.

Alipotafutwa Masogange alikuwa na haya ya kusema: “Sijaanza kusikia tuhuma hizo leo lakini mimi si mtu wa mambo ya Kiswahili ujue, nimetoka kwenye familia ya kichungaji.”
Powered by Blogger.