BARUA ZA NIYONZIMA AMBAZO MANJI AMESEMA TIBOROHA ALIZIFICHA ILI MCHEZAJI HUYO AFUNGIWE
Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji, leo amesema aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Dk
Jonas Tiboroha alikuwa akificha barua za kiungo Haruna Niyonzima
alizokuwa akiziwasilisha kwa ajili ya utetezi au taarifa kuwa anatakiwa
timu ya taifa ya Rwanda.
"Baada
ya kuupitia uamuzi wa Kamati ya Nidhamu kuamua sababu kuvunja mkataba
kati ya klabu Yanga na mchezaji Haruna Niyonzima, nilihisi kulikuwa kuna
kasoro hasa kwa mchezaji anayelipwa mshahara wa Sh milioni 6 anaweza
vipi kupuuzia maisha yake na kuanzisha mgogoro usiokuwa na tija kwa
maisha ya kipato.
"Niliamua
uchunguzi wa ndani ufanyike katika suala hilo zima na mwisho, Jonas
Tiboroha alibainika kuwa hakuwasilisha ushahidi ya mawasiliano sahihi
kwa Kamati ya Nidhamu kuhusiana na Haruna Niyonzima, hali iliyosababisha
kamati kuchukua uamuzi ambao haukuwa sahihi kwa sababu;
"Kulifanyika
mambo ambayo hayakuwa sahihi, mfano barua za Niyonzima kutoka kwa
Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa) ambazo zilitumwa kwa TFF na
kupokelewa kama ambavyo Azam FC walipokea ya mchezaji wao kupitia kwa
Afisa Mtendaji Mkuu wao.
"Lakini
barua ya Niyonzima kuja Yanga, ilionekana haikupokelewa kama ilivyokuwa
kwa barua yake ya utetezi na ile ya kuomba radhi alizoandika, nazo
zilipokelewa lakini hazikuwasilishwa kwenye kamati ya nidhanmu na hili,
mhusika ni Tiboroha. Ukiachana na kamati kufanya uamuzi usio sahihi,
hili pia limemjengea mchezaji chuki kubwa kwa wanachama na mashabiki.
![]() |
| FERWAFA ILITOA OMBI LA NIYONZIMA KWENDA KUCHEZA MICHUANO YA KIMATAFA KUWANIA KUCHEZA KOMBE LA DUNIA DHIDI YA LIBYA |
![]() |
| FERWAFA WALIMUOMBEA NIYONZIMA RUHUSA KWA AJILI YA CHALENJI, AWALI ILIELEZWA ALIKWENDA KUSHIRIKI CHALENJI BILA YA RUHUSA... |
![]() |
| BARUA NYINGINE YA NIYONZIMA INAYOELEZWA KUFICHWA... |
![]() |
| KITENGO CHA TIBA, TIMU YA TAIFA YA RWANDA KILIANDIKA KUHUSIANA NA MAJERAHA YA NIYONZIMA |






Post a Comment