Wema, Jokate waungana kummaliza Diamond...Wote waonesha mahaba niue kwa Kiba
Kiba akiwa na Jokate.
WAREMBO ‘classic’ ambao ni zao la Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu na Jokate Mwegelo wamedaiwa kuungana pamoja kumsapoti staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba ‘King Kiba’ ili kumfunika mpenzi wao wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kiba akiwa na Wema Sepetu
Wema na Jokate ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kulitumikia penzi la Diamond, Desemba 26, mwaka huu walipanda kwenye jukwaa la Kiba na kuanza kuonyesha uwezo wao wa kucheza muziki mbele ya mashabiki waliokuwa wamefurika ndani ya Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar.
Wawili hao walikuwa gumzo baada ya kuonekana kwa nyakati tofauti wakipanda jukwaani hapo na kukumbatiana na Kiba kisha kusalimiana na mashabiki huku wakicheza muziki kwa pamoja na staa huyo ambaye alikuwa akiwachombeza kwa maneno matamu kila mmoja alipopanda kujumuika naye.
Jokate ambaye sasa ndiye anayemmiliki Kiba kimahaba, alikuwa wa kwanza kuingia ukumbini hapo na kuketi kiti cha mbele tangu Kiba alipoanza kufanya makamuzi yake akiwa anamshuhudia na kupiga makofi.
Wema yeye aliingia na kundi la marafiki zake kama Petit Man, Idris Sultan, Aunt Ezekiel na wengine kibao ambao nao kwa pamoja waliketi meza ya mbele jirani kabisa na walipokuwa kina Jokate, hivyo Kiba baada ya kuwaona alianza kuwasifia na muda ukafika Wema akapanda jukwaani hapo huku Jokate akionesha tabasamu linaloashiria kwamba wako pamoja kumsapoti Kiba.
“Wameungana pamoja kummaliza Diamond. Si unajua Diamond alileta maneno mabovu baada ya kuwamwaga, sasa na wao wanaungana kumsapoti Kiba ili kumuonesha Diamond umuhimu wao,” alisikika mdaku mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Kabla ya Kiba kufunga na kushuka jukwaani hapo, aliwashukuru kwa pamoja mashabiki wake kwa kujitokeza kumpa sapoti kubwa lakini pia pongezi za kipekee alizielekeza kwa Jokate na Wema ambao waliweza kupanda jukwaani na kuonyesha hali ya kumpigania kwa kila namna.
“Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru nyinyi nyote mliojitokeza kuja hapa kwa ajili ya kusherehekea nami mwaka mmoja tangu nirejee kwenye gemu, ahadi yangu ni kuhakikisha naendeleza mapambano kiasi cha kutowaangusha kwa mara nyingine, nitoe pongezi zangu za pekee kwa Wema na Jakate ambao mmekuwa mstari wa mbele kuhakikisha shoo hii inafanikiwa kwa kukusanya idadi kubwa ya watu kama leo tunavyoona mambo yamekwenda vizuri,” alisema Kiba.
Post a Comment