Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo ni Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe Magufuli leo ametangaza baraza lake la mawaziri ambalo atashirikiana nalo katika kuendesha serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha wanasimamia na wanatimiza kile walichokiahidi wakati wanaomba ridhaa ya uongozi kwa wananchi.Katika suala linalohusu michezo, Dr. Magufuli amemteua Nape Moses Nnauye kuwa Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo na Naibu Waziri wa Wizara Hiyo ni Anastazia Wambura.
Nnauye ni Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya CCM ameteuliwa kuwa Waziri kwa mara ya kwanza ambapo kabla ya wadhifa huo alikuwa Katibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mtandao huu (shaffihdauda.co.tz) unamtakia kila la kheri Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika kuhakikisha anasimamia wizara hiyo kikamilifu na kuhakikisha michezo inapiga hatua kutoka alipoicha Waziri aliyemaliza Muda wake Dr. Fenella Mukangara.

Post a Comment