TIMU IPI KUTOKA EPL ITAUNGANA NA MAN CITY KUFUZU HATUA YA MTOANO YA MICHUANO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE?
PSV nayo ni timu inayo toka kundi B pamoja na timu hizi, yenyewe itakuwa nyumbani kucheza na CSKA Mosco, PSV pia inanafasi ya kusonga mbele hivyo inazidi kuchagiza ugumu wa timu gani itasonga mbele na ipi itaaga mashindano haya kwenye hatua ya mapema.
Kesho itakuwa ni zamu ya timu nyingine mbili za England hapa nazizungumzia Arsena na Chelsea ambazo pia zipo katika hali tete. Endapo timu hizi zitafungwa basi moja kwa moja zitakuwa zimeyaaga mashindano ya UEFA Champions League msimu huu.
Manchester City ndiyo timu pekee kutoka England ambayo tayari imejihakikishia nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo, timu nyingine tatu za Man United, Arsenal na Chelsea zenyewe zinasubiri hadi mechi zao za mwisho ili kuamua hatma zao.
Hapa nimejaribu kukuonesha nasafasi ya timu za England kwenye michuano ya UEFA Champions League, je ni timu gani zitaungana na Manchester City kusonga mbele kwenye michuano hiyo?
Game: Chelsea vs FC Porto (Stamford Bridge)
Chelsea, Porto na Dynamo Kiev zote zina nafrasi ya kufuzu kwenye hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa Ulaya lakini Dynamo Kiev inanafasi kubwa kwasababu mchezo wake wa mwisho itacheza dhidi ya timu dhaifu ya Israel Maccabi Tel Aviv na inapewa nafasi kubwa ya kutwa ponti zote tatu kwenye mchezo huo.
Mechi kati ya Chelsea dhidi ya FC Porto ili Chelsea ifuzu kwa ajili ya hatua ya mtoano inahitaji ushindi ili kuongoza kundi G, FC Porto kwa upande wao ushindi pekee ndio utawahakikishia nafasi ya kusonga mbele (kama Dynamo Kiev itashinda dhidi ya Maccabi).
Game: Olympiacos vs Arsenal (Karaiskakis Stadium)
Kwenye kundi F, timu mbili zinapambana kuwania nafasi moja kwasababu Bayern Munich yenyewe imeshafuzu kama timu inayoongoza kundi hilo.
Ili Arsenal isonge mbele ni lazima ishinde dhidi ya Olympiacos, lakini si lazima ishinde tu bali ushindi wa kuanzia goli 2-0, 3-1, au matokeo mengine yenye magoli mengi zaidi ya hayo ndiyo yataisaidia Arsenal kusonga mbele.
Game: Wolfsburg vs Manchester United (Volkswagen Arena)
Group B ni group gumu na lenye upinzani wa aina yake, timu tatu zinawania nafasi mbili za kufuzu kwa ajili ya hatua ya mtoano. Timu hizo ni Manchester United, Wolfsburg pamoja na PSV Eindhoven
Manchester United inahitaji ushindi pekee ili kusonga mbele bila kuathiriwa na matokeo ya timu nyingine na hiyo inamaanisha Wolfsburg itatupwa nje ya michuano ya Champions League na kudondokea kwenye Europa League kama PSV itapata ushindi wa nyumbani dhidi ya CSKA Moscow.
Mchanganuo wa nafasi ya kusonga mbele kwa timu za kundi B upo kama ifutavyo;
Man United ikishinda na PSV ikishinda = Man United inaongoza kundi na PSV itashika nafasi ya pili kutinga kwenye hatua ya 16 bora.
Man United ikishinda na PSV ikapoteza = Man United itaongoza kundi wakati Wolfsburg itakuwa nafasi ya pili kufuzu hatua ya 16 bora.
Man United ikitoka sare halafu PSV ikatoka sare au ikapoteza = Wolfsburg itaongoza kundi Man United itashika nafasi ya pili na kufanikiwa kusonga mbele.
Man United ikipoteza, PSV ikatoka sare = Wolfsburg itaongoza kundi huku PSV ikifatia kwa kushika nafasi ya pili.
Man United ikipoteza, PSV ikipoteza = Wolfsburg itaongoza kundi, Man U nayo itafuzu ikiwa nafasi ya pili kutoka kwenye kundi kwenda hatua ya 16 bora.
Post a Comment