Pedeshee aapa kuvunja uchumba wa dida
Pedeshee maarufu jijini Dar anadaiwa kuapa kuvunja uchumba wa Mtangazaji wa Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ mara tu baada ya kutangaza kuvalishwa pete ya uchumba hivi karibuni na mwanaume ambaye hakutaka kumuanika.
Habari kutoka kwa chanzo chetu makini
zilieleza kwamba, pedeshee huyo amekuwa akimpa Dida vitisho kuwa
mwanaume ambaye atamuoa hatakuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yake hivyo
anaamini yeye ndiye anayeweza kumpa chochote anachotaka na si mwingine.
“Jamaa
anajitapa hata kwa baadhi ya ndugu wa Dida kuwa mwanaume ambaye anataka
kumuoa Dida hana vigezo vya kuweza kutatua matatizo yake hivyo yeye
yupo tayari kuvunja uchumba huo kwa gharama yoyote,” kilisema chanzo
hicho.
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, gazeti hili lilimtafuta
mtangazaji huyo kwa njia ya simu ambapo alikiri kujitokeza kwa mwanaume
huyo lakini alisema kuwa mwanaume anayemuoa anaweza kukidhi mahitaji
yake.
“Mchumba wangu ni mtu mwenye maisha yake wala si mbabaishaji
kama baadhi ya watu wanavyodhani na wala sihitaji kabisa ofa ya
mwanaume mwingine yeyote,” alisema Dida.
CHANZO: GPL
Post a Comment