ad

ad

MTANZANIA AWEKA REKODI YA KUKOSA PENALTI TATU KATIKA MECHI MOJA KOMBE LA FA LA AZAM TV


Ally Haji Mbwela wa Might Elephant ameweka rekodi ya aina yake katika soka nchini baada ya kukosa penalti tatu katika mechi moja.

Mbwela amekosa penalti hizo tatu katika mechi ya Kombe la FA linalodhaminiwa na Azam TV katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Might Elephant ilimaliza mechi dhidi ya JKT Mlale kwa sare ya mabao 2-2. Penalti zikaanza na Mbwela alikuwa kati ya waliokosa penalti mbili za mwanzo.

Baada ya hapo, wachezaji waliofuatia hadi makipa walipata na kufanya matokeo yawe 7-7. Wakatakiwa wachezaji kuanza kurudia.

Mchezaji wa kwanza wa Mlale ambaye alikosa penalti ya mwanzo alifunga, mchezaji aliyefuatia wa Might Elephant akawa ni Mbwela ambaye alikosa.


Wakati JKT wakishangilia, mwamuzi alisema kipa alitoka. Hivyo Mbwela akapewa nafasi ya kurudia penalti nyingine ambaye ilikuwa ya tatu kwake, akapiga, nayo akakosa na Might Elephant ikawa imeng’olewa.
Powered by Blogger.