T.B JOSHUA ATUA DAR...PICHA ZIPO HAPA
Rais mteule wa awamu ya tano, Dkt
John Pombe Joseph Magufuli alimpokea Mhubiri wa kimataifa kutoka
Nigeria TB Joshua Uwanja wa ndege Dar jioni jana. Mhubiri huyo aliyekuja
na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli
akiapishwa.
Rais mteule wa awamu ya tano, Dkt
John Pombe Joseph Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli
wakibadilishana mawazo na Mhubiri wa kimataifa kutoka Nigeria TB Joshua
mara baada ya kuwasili nchini jioni jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akimlaki Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini
Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni jana. TB Joshua ametua jijini
Dar es salaam tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano
Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea na Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini
Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni jana. (Picha na Freddy Maro)
Mtume TB Joshua wa Kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria
ametua jijini Dar es salaam jana tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais
wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha.
TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt. Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.

Post a Comment