Papa Francis: Dini isitumiwe kuvuruga amani
Papa
Francis: Dini isitumiwe kuvuruga amani
PAPA Francis
wa Kwanza ameongoza ibada ya misa ya kwanza leo barani Afrika akiwa nchini
Kenya ambayo imehudhuriwa na maelfu ya watu
katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi akisisitiza umuhimu wa kuheshimu
familia katika jamii.
Awali katika
mkutano na viongozi wa dini mbalimbali, alisema dini haifai kutumiwa
kuvuruga amani kwani “Mungu ni Mungu wa
amani.
"Jina
lake takatifu halifai kutumiwa kutetea chuki na mauaji. Ninajua kwamba
mashambulio ya Westgate, Chuo Kikuu cha Garissa na Mandera bado
hayajasahaulika. Na sana, vijana wamekuwa wakiingizwa na kufunzwa itikadi kali
kwa jina la dini, kupandikiza woga na kuvunja umoja katika jamii,” alisema.
"Ni
muhimu sana tuwe manabii wa amani, watu wa amani wanaokaribisha wengine kuishi
na amani, umoja na kuheshimiana. Mungu na akaguse mioyo ya wanaohusika katika
mauaji na ghasia, na azipe imani familia na jamii zetu."
Post a Comment