Mchumba Jack Dustan ajitutumua na ka-Vitz
BAADA
ya kuhakikishiwa ndoa, mchumba wa mrembo aliyejipatia jina kupitia
Shindano la Maisha Plus Season 11, Jacqeuline Dustan, Hamis Ally
amejitutumua kwa kumnunulia mkewe mtarajiwa huyo kagari aina Toyota
Vitz.
Wawili
hao wanatarajia kufunga ndoa mwanzaoni mwa mwaka ujao na baada ya kila
kitu kwenda sawa ikiwa ni pamoja na kulipiwa mahari, Hamis aliona atoe
zawadi hiyo ili kumuonesha Jack kuwa amefurahi kuona ndoto zake za
kuishi naye zinaelekea kutimia.
Akizungumza
na Ijumaa mara baada ya kunaswa na gari hilo, Jack alisema: “Yaani
hakuwa akiamini kwamba tutafi kia hatua hii na ndiyo maana amenipa hii
zawadi ya gari. Ni gari f’lani niliyokuwa naipenda sana.”
Post a Comment