ad

ad

HADITHI: ... RAHA YENYE MAUMIVU SEHEMU: 02


MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
ILIPOISHIA:
Alikiweka kile kikalatasi na shilingi laki saba kwenye mfuko wa suruali wa kijana Augustino Tamilway kisha alimpiga busu kwenye shavu na kuondoka kuwahi usafiri wa ndege uwanja wa ndege wa kimatafa wa Kilimanjaro (KIA)
Aliwasiri kiwanjani nusu saa kabla ndege haijaondoka na kufuata taratibu zote zilizomwezesha kukamilisha taratibu za usafiri na saa kumi na mbili juu ya alama Mam’ kubwa au mama Teddy aliiaga anga ya Tanzania.
SASA ENDELEA…
******
Kijana Augustino Tamilway au kama wengi wapendavyo kumwita Tino aliposhtuka usingizini alijishangaa kujikuta yupo peke yake kitandani. Alipepesa macho yake akijua labda jimama amekwenda kuoga lakini alikumbuka jana alimweleza ana safari alfajiri.
Aliona yule mama alimdanganya na kumkimbia hata bila ya kumuasha, lakini alijipa moyo kuwa kuna chenji ambazo hakumrudishia Mam’ Kubwa wakati akimtuma pombe ambazo si chini ya elfu nane alijua zitamtoa kwa asubuhi.
Lakini wazo lilimjia huenda yule jimama amezichukua zile hela zitazomfanya aone siku ngumu kwake wazo lake la kwanza ni kwenda kuziangalia zile hela zake kama zimo au la.
Alinyanyuka hadi sehemu aliyoweka suruali yake kitu kingine kilichomtia hofu ni ile hali ya suruali ilivyo kuwa ni tofauti na yeye alivyoiweka. Aliichukua suruali na kuingiza mkono mfuko alishangaa mkono kukutana na uzito alishika vizuri kilichokuwemo na kukitoa hakuamini macho yake zilikuwa pesa nyingi zilizo zungurushiwa kalatasi ndogo nyeupe.
Alizirudisha zile pesa mfukoni na kukisoma kile kikalatasi kilichokuwa na maneno matamu ambayo yalimfanya azitoe zile hela na kuzihesabu zilikuwa laki saba. Tino alishukuru Mungu kweli unaweza kulala maskini na ukaamka tajiri ule usemi ulijidhihirisha kwake.
Katika kitu alichokuwa akikitafuta maishani mwake ni kupata mtaji ambao utamsaidia maishani yeye katika kuhangaika aliomba siku moja apate laki moja ya mtaji lakini siku ile amepata laki saba. Alijua huo ndio mwisho wa kufanya kazi za kuajiliwa alipanga kukimbila jijini Dar kuanzisha biashara ya mitumba.
*****
Augustino Tamilway baada ya kupata kiasi kile kikubwa cha pesa hakuwa na haja ya kupoteza muda aliamua siku ya pili kukimbilia jijini Dar bila kuwaaga watu zaidi ya rafiki yake mkubwa Dani kuwa anakwenda Dar kujaribu maisha. Lakini hakumweleza kuwa ana pesa za kumfanya asiyumbe kimaisha katika jiji linalo aminika ndilo linaloongoza kwa matumizi ya pesa kila kitu kinanunuliwa mpaka uchafu.
Aliondoka jijini Arusha majira ya saa kumi na mbili na basi la Dar express na kuwasiri jijini majira ya saa tisa mchana hakuwa mgeni wa jiji alikwenda kwa rafiki yake Flibert aliyekuwa anakaa Keko Mwanga.
Kwa bahati alimkuta rafiki yake ambaye alikuwa akifanya kazi kampuni ya Plasitic. Hapo ndipo Tamilway alipoanza maisha yake kwa kuulizia biashara gani zinazofaa alielekezwa na kuanza na biashara ya kutandaza chini mtaa wa Kongo .
Alijikuta akipata faida kila kukicha na kufikia hatua ya kusajili watu kumuuzia biashara zake. Alijikuta akipata pesa zilizomfanya aongeze biashara zingine ikiwa pamoja na kununua fremu ya kuuzia biashara zake zilizompa utajiri wa haraka sana.
Wakati huo alikuwa ameishahama kwa rafiki yake Filbert na kupanga chumba chake mwenyewe maeneo ya Temeke Wailes.
********
MIEZI MITATU BAADAYE JIJINI LONDON UINGEREZA

Mabadiliko ya hali ya mam’ kubwa au mama Teddy yalimtia wasiwasi baada ya kupoteza siku zake kwa muda wa miezi miwili kitu kilichomtia wasiwasi na kumfanya aende hospital kuangalia afya yake ajue ile hali ya kutokuziona siku zake inatokana na nini.
Baada ya vipimo vyote ilionekana Mam’ kubwa ni mjamzito wa miezi miwili kitu kilicho mshtua na kuuliza mara mbilimbili.
"Ni kweli usemayo dokta?"
"Kwa nini nikudanganye wewe ni ujamzito wa miezi miwili."
Baada ya kusikia taarifa ile ilimfanya arudishe kumbukumbu zake nyuma na kujiuliza ni mwanaume gani aliye kutana naye miezi mitatu nyuma. Jibu lilikuwa ni Tino kwani ndiye anayekumbuka alikutana naye siku za hatari lakini hakuwa na wasiwasi kwa kujua muda ule hawezi kuzaa tena.
Toka afike jijini London akuwahi kutembea na mwanaume kwa kupindi cha mwezi mzima, kwa kuwa alikuwa bize ma masuala ya biashara. Mara nyingi alipenda kufanya starehe baada ya kumaliza pilikapilika zake za biashara.
Kama ujauzito ungekuwa wa mwezi mmoja angejua ameupatia pale lakini wa miezi miwili lazima alijua ameupatia Tanzania tena jijini Arusha na aliyempatia si mwingine ni Tamilway yule muhudumu wa hotel ya New Arusha.
Pamoja na kupata mshituko haukuwa wa kujuta bali wa furaha kwani ni baada ya miaka 19 toka ajifungue mtoto wake wa kike ambaye kwa sasa anakimbilia miaka 20. Japo alikuwa na hamu ya kupata mtoto mwingine lakini hakubahatika pamoja na kumsaka kwa udi na uvumba lakini aliambulia patupu.
Alitumia dawa za mwanga na kiza zote zilidunda pamoja na kujitahidi kubadilisha wanaume kila kukicha. Alijua Mungu alimpa mtoto mmoja wa kike hata hivyo alimshukuru Mungu kwa kumpatia mtoto wa kike kwani wapo waliokosa kabisa.
Ilikuwa ni furaha isiyo na kifani baada ya kupata uhakika kuwa ana ujauzito wa miezi miwili. Aliamua kubakia Uingereza ambako alipanga angekaa kwa muda na kutimkia Marekani ambako angeendelea kuutunza ujauzito wake karibu na hospitali kubwa duniani ili kuhakikisha hampotezi mwanaye.
Aliogopa kurudi Afrika kwa kuwa wanawake walio wengi upoteza watoto kwa sababu za kizembe. Hata mwanaye anayesoma Hi-lavel alimwagiza amalizapo mtihani wa kidato cha sita amfuate mama yake ulaya.

MIEZI TISA BAADAYE

Muda wa kulipo timu aljifungua salama mtoto wa kiume aliye kuwa na afya njema, aliyempa jina la baba yake mzazi Malon. Baada ya miezi sita ndipo alipoamua kurudi jiji Dar, siku aliyofika hakupumzika alikwea ndege hadi jijini Arusha kumtafuta kijana Tamilway ambaye alimuona anamfaa kuwa mumewe japo kijana mdogo kwa sababu penzi halichagui umri.
Mam’ kubwa au kwa sasa analipenda aitwe mama Malon aliwasiri Arusha majira ya saa kumi jioni na kwenda moja kwa moja Hotel ya New Afrika na kumuulizia Tamilway. Kutokana na muda mrefu kupita aliwakuta wafanyakazi wageni, walisema hawamjui lakini alijaribu kutafuta wenyeji ambao nao walimjulisha kuwa hayupo hata uondokaji wake ulikuwa wa ghafla hivyo hawajui yupo wapi kwa muda ule.
Majibu yalimkatisha tamaa na kuamua kurudi jijini akiwa amelowa na kujiona kama mtu aliyepotelewa koti lake wakati wa baridi kali. Alijua huo ndiyo muda wake wa kutulia baada ya kupata mtoto na kumfanya mume mwanaume aliyemzalisha.
Kauli ya mwanaye siku zote ilimuumiza sana pale alipomuonya mama yake tabia ya kuchanganya wanaume vijana na wazee bora atafute mtu mmoja atulie naye tena anayejiheshimu kuliko kurukaruka ipo siku watachangia mwanaume watashindwa kutazamana.
Baada ya kupata ujauzito ule alijua jawabu ya kilio cha mwanaye limepatika lakini siku zote wa moja havai mbili. Alirudi Dar akiwa amechoka aliamua kumlea mwanaye kwanza hata baadhi ya biashara zake alizimamisha kwa ajili ya kumlea mwanaye ambaye alijua ndiye kichwa cha familia.
Malon alipo fikisha miaka miwili alipelekwa shule ya kulelea watoto iliyo nchini Marekani ambako alimpeleka ili yeye aendelee na biashara zake pamoja na kulipa hela nyingi lakini alijua ndiyo sehemu iliyo salama ambako mtoto hupata malezi na elimu ya hali ya juu.
Nini Kitaendelea ili kuyajua yote endelea kufuatulia.
Bado naendelea na usajili katika Whatsapp Group kwa Ths 2500 kwa mwezi. Baada ya mwezi wa Ramadhani Chombezo mtakalolichagua linaanza baada ya hapo sitapokea mtu tena kwa vile nimetoa muda wa kutosha.
Powered by Blogger.