Gari la Wema siri nje!, ALIYEMUONGA ATAJWA
MAMBO
hadharani! Siku chache baada ya Miss Tanzania 2006/07 ambaye pia ni
supastaa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Abraham Sepetu kujigamba
amenunua kwa pesa zake gari jipya aina ya Range Rover Evoque 504 lenye
thamani ya dola za Kimarekani elfu 90 (karibia shilingi milioni 200),
siri kubwa imevuja kuhusu gari hilo.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu ambacho kiliomba kuhifadhiwa jina ili
kisionekane kimbeya, gari hilo la kifahari halijanunuliwa na Wema bali
amepewa na mwanaume mmoja Mkongo ambaye awali, alikuwa na uhusiano wa
kimapenzi na staa mwingine wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Massawe.

MSIKIE HUYU
“Jamani nataka kuwapa umbeya lakini naomba msinitaje! Sawa?”
Amani: “Sawa, lete habari ya huo umbeya wako.”
Chanzo: “Mliandika kwamba, Wema amenunua gari la Range sijui. Mkasema amelinunua kwa shilingi kama milioni mia mbili.”
Amani: “Sawasawa kabisa. Lete maneno.”
Chanzo: “Sasa mimi nina habari kwamba, lile gari Wema amepewa na yule mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi wa Jack Wolper.”
KACHEZEWA KAMA WOLPER?
“Lakini
mimi naogopa sana kwani kuna habari zinasambaa kwa kasi kwamba, ndani
ya miezi miwili, Wema hatakuwa tena na hilo gari. Litarudishwa kwa
mhusika.
“Nasikia
lile gari, kwanza ni kweli ni jipya. Lakini liko kwa dalali sokoni.
Sasa watu wanaojua habari za mjini wanasema kuwa, Mkongo aliongea na
dalali, wakaelewana kwa kumpa pesa kidogo, ikatengenezwa dokyumenti
ambazo zinamwonesha Wema ni mmiliki halali wa gari.
“Nadhani
wanaposema Wema hatakuwa na lile gari kwa miezi miwili mbele, huenda
watamchezea kama alivyochezewa Wolper mwaka ule na lile gari alilohongwa
na yule jamaa yake, Dallas (Abdallah Mtoro). Wolper alipewa gari na
dokyumenti zake, kumbe lilikuwa mazabe,” kilisema chanzo hicho.
WEMA ASAKWA
Kama
kilivyosema chanzo kuwa, kisitajwe ili kisije kikaonekana ni kimbeya au
kinasema uongo, ili kuweka sawa mizani ya habari hii, Amani lilimsaka Wema kwa njia ya simu na kumuuliza.
Wema
alisomewa mashtaka yote mpaka mwisho kwa kuambiwa hajanunua yeye lile
gari bali lina nguvu ya mkono wa mwanaume ambapo naye alifunguka kidogo
kwa kusema:
“Ni
kweli, inawezekana kuna mkono wa mtu mwingine lakini mimi nitakupigia
baadaye kidogo ili tuongee vizuri,” alisema Wema kwa kifupi kisha
akakata simu.
SIKU ZAKATIKA
Hiyo
ilikuwa ni Jumatano ya Novemba 4, 2014. Ilipofika Jumatatu ya Novemba
9, mwaka huu, mwandishi aliamua kumpigia simu Wema, hakupokea.
Jumanne,
juzi, mwandishi alimpigia simu tena lakini si tu kwamba hakupokea, bali
zaidi sana hakuwa hewani kabisa mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni.
WOLPER SASA
Amani liliamua kumsaka Wolper kwa njia ya simu na kumuuliza kama ana habari za Mkongomani wake kumpa gari Wema ambapo alisema:
“Mimi
nitajulia wapi jamani! Sijui lolote lile. Kwanza huyo Mkongo mnayemsema
sijui yuko wapi siku hizi. Ana maisha yake na mimi nina maisha yangu.
Teh...tehe...teheee...”
TURUDI NYUMA
Novemba
Mosi, mwaka huu, Wema aliangusha bethidei ya nguvu iliyofanyika kwenye
ukumbi mmojawapo ndani ya Jengo la Millennium Tower jijini Dar.
Katika
hafla hiyo, Wema alishika kipaza sauti na kusema: “This is my new brand
car, yaani ni jipya la mwaka 2015. Hakuna kenge yeyote anayeweza
kufuata nyendo zangu. Na yule ambaye alikuwa akijigamba eti alinipa
zawadi ya gari la elfu 30 nini na nini na hili aseme sasa, maana mimi si
wa kuhongwa kila kitu.”
Akaendelea:
“Naomba niwaambie kuwa, hadi nalifikisha hapa, hili gari nimetumia
zaidi ya dola elfu 90 za Kimarekani. Sijahongwa na mtu, ni pesa zangu
kwa nguvu zangu mwenyewe. Nawaomba mpande ndani mshuhudie ziro kilometa
(halijatumika).”
Kauli
hiyo ilionesha wazi kumlenga Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
ambaye aliwahi kumzawadia Wema gari (Nissan Murano) lenye thamani ya
shilingi milioni 30 miaka miwili iliyopita.
CHANZO: GPL


![wolper[1]](http://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/wolper1.jpg)
Post a Comment