Dina: Wakati wa kina Wema umekwisha
CHIPUKIZI anayekuja juu na ambaye alifanya vyema katika Filamu ya Nakufa kwa Ajili Yako, Nasra Mohamed ‘Dina’ amesema wakati wa mastaa wenye majina makubwa kama Wema Sepetu umepita kwani wapo wasanii wapya wanaopiga kazi kiuhakika.
Akizungumza na juzikati, Dina alisema mastaa kama Wema, Lulu, Aunt na wengineo ni wa kuwekwa kando, kwani muda wao umeisha, watoe nafasi kwa wengine kuingia kazini.
“Mimi nataka mastaa wakivuma basi wawe wanafanya kazi kisawasawa, siyo wanabakia kuuza sura tu kazi hawafanyi, wawekwe kando kama inavyokuwaga kwa wacheza mpira, waingie timu za wachezaji wakongwe, yaani maveterani,” alisema.
Post a Comment