ad

ad

HATIMAYE ZAHA AFUNGUKA KUHUSIANA NA UHUSIANO WAKE NA BINTI WA DAVID MOYES

 Kiungo nyota wa Crystal Palace, Wilfred Zaha amefunguka na kusema kamwe hakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti wa aliyekuwa Kocha wa Manchester United, David Moyes.

Zaha amesema ajabu zaidi, hajawahi hata kukutana na Lauren ambaye alizushiwa kwamba alikuwa na uhusiano naye kimapenzi, hali iliyosababisha Moyes kutompanga.

Hata hivyo, amesema alishangazwa kusifikia Moyes akimuambia hakuwa tayari kwa ajili ya Ligi Kuu England.

“Ilinishangaza sana, nakumbuka aliniambia hivyo jambo ambalo sikukubaliana nalo hata kidogo. Haikuwa sahihi,” alisema Zaha mwenye asili ya Ivory Coast.

Zaha alitua Manchester United akitokea Crystal Palace, lakini siku chache baadaye Kocha Alex Ferguson alitangaza kustaafu.

“Nilijisikia vibaya sana baada ya Ferguson kutangaza kustaafu, ndiyo nilikuwa nimefika na nilikuwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri nikiwa chini yake. Lakini sikuwa na uwezo wa kumshawishi aendelee kubaki,” alisema Zaha.

Ameendelea kusisitiza kwamba anaishi maisha mazuri Crystal Palace na ana furaha kubwa ukilinganisha na alivyoishi Manchester United.
Powered by Blogger.