NYOSSO AFUNGIWA KUCHEZA SOKA MIAKA MIWILI, APIGWA FAINI YA NOTI NOTI 200 ZA SH 10,000
Kikao cha Kamati ya nidhamu ya TFF kilichokutana ndani ya saa 72,
kimefungia nahodha wa Mbeya City, Juma Said Nyosso kucheza soka kwa miaka miwili.
Pamoja na miaka hiyo miwili, Nyosso ametozwa faini ya Sh milioni mbili kutokana na kitendo chake cha kumshika makalio nahodha wa Azam FC, John Bocco.
Hii ni mara ya pili kwa Nyosso kushiriki katika tukio, mara ya kwanza
alimtomasa Elius Maguli wakati akiichezea Simba.
Kutokana na picha ilivyochapishwa kwenye gazeti la Championi na
SALEHJEMBE akafungiwa kucheza mechi nane.
Baada ya hapo, Nyosso aliwaomba radhi Watanzania pamoja na wapenda soka wote, lakini bado amerudia.
Post a Comment