MANCHESTER UNITED YAFANYA USAFI, CHICHARITO, EVANS KWAHERI DE GEA AKWAMA
Javier Hernandez ‘Chicharito’ wakati akikipiga Real Madrid kwa mkopo
Kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili vilabu vya soka barani Ulaya klabu ya Manchester United imeendelea kufanya marekebisho ya kikosi chao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa kikosini wachezaji wasio na nafasi kikosini.
Katika siku mbili hizi za mwisho, imeelezwa kuwa uhamisho wa golikipa wa Manchester United David De Gea kwenda Real Madrid umekwama baada ya jana usiku dirisha la usajili nchini Hispania kufungwa huku golikipa huyo akiwa tayari yupo nchini kwao akisubiri dili likamilike ili aweze kujiunga Madrid. Taarifa zinasema Manchester iliitumia klabu ya Madrid ‘documents’ ambazo walishindwa kuzifungua ili kukamilisha usajili huo, hivyo De Gea ataendelea kusalia Manchester hadi utaratibu mwingine utakapofanyika ikiwa ni pamoja na kuomba ruhusa ya FIFA.
Javier Hernandez karuhusiwa kuondoka, na sasa anaelekea Bayern Leverkusen ya Ujerumani, sanjari na Adnan Januzaj ambaye amejiunga na Borusia Dortmund ya ujerumani pia kwa mkopo wa msimu mzima.
Wachezaji hao wanaungana na mlinzi John Evans ambaye aliondoka kikosini hapo kwa ada ya pauni milioni 6 kujiunga na klabu ya Westbromwich Albion inayoshiriki ligi kuu nchini uingereza.
Wakati huo huo Manchester United inakamilisha usajili wa mshambuliaji Mfaransa kutoka katika klabu ya Monaco, Anthony Martial (19) kwa ada inayotarajiwa kufikia pauni 58.
Post a Comment