ad

ad

Emmanuel Mbasha aachiwa huru




By Hadija Jumanne, Mwananchi
Dar es Salaam.Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Emmanual Mbasha (32), jana ameangua kilio baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Ilala huku mke wake, Flora amesema yuko tayari warudiane endapo ataomba radhi.
Mbasha alimwaga chozi muda mfupi baada ya kutoka katika chumba cha Mahakama alipopandishwa kizimbani kusomewa hukumu.
Mshtakiwa huyo  ameachiwa huru dhidi ya kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha kosa.
Mwimbaji huo ambaye kabla ya kutolewa kwa hukumu  hiyo alionekana hana furaha, alifikia uamuzi huo wa kulia mara tu baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo, ambapo alipotoka nje ya chumba cha mahakama alipiga magoti chini huku akiinua mikono juu na kulia kwa sauti  huku akisema ‘mungu ni mwema’.
Mbasha  anakabiliwa na mashtaka mawili ya kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17  huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria
Kesi hiyo namba 186 ya mwaka 2014, imeendeshwa kwa mwaka mmoja na miezi miwili na kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo Juni  17 mwaka 2014.
Akisoma hukumu hiyo leo, hakimu  Mkazi Flora Mujaya alisema mahakama imemuachia huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha  kosa lililokuwa likimkabili.
“Mahakama yangu imemuachia huru Mbasha  baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha kosa  ”alisema Hakimu Mujaya.
Hakimu Mujaya alisema mahakama hiyo imetoa uamuzi huo baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi sita  wa upande wa mashtaka vikiwemo vielelezo vilivyotolewa  mahakamani hapo kama ushahidi.
Hukumu hiyo, ilipaswa kutolewa wiki iliyopita , lakini  iliahirishwa hadi jana kwa sababu hakimu huyo ambaye ametoa hukumu  hiyo leo alikuwa likizo .
Mke wa Mbasha, Flora alisema yeye na familia yake wanaheshimu maamuzi yaliyotolewa na Mahakama  dhidi ya Mbasha na kwamba anaiomba familia yake ikubaliane na maamuzi  hayo na suala la kukata rufaa lisiwepo.
“Mimi na familia yangu tunaheshimu uamuzi wa mahakama na ninaiomba familia yangu ikubaliane na uamuzi huu  uliotolewa na mahakama na suala la kukata rufaa lisiwepo kwani uamuzi wa mwisho upo katika familia” alisema Frola alipotafutwa kwa simu.


Powered by Blogger.