VITA AZAM NA GOR MAHIA NANI KUTAWAZWA MFALME KAGAME CUP LEO
Leo ndio Leo Fainali
ya Kombe la Kagame kati ya Azam FC dhidi ya Gor Mahia ya Kenya
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
Azam
FC yenye beki imara ambayo haijaruhusu hata bao moja mpaka hatua hii
imeingia fainali baada ya kupata ushindi dhidi ya KCCA kwa bao 1-0 huku
Gor Mahia ikiwa imeingia fainali baada ya ushindi dhidi ya timu ngumu ya
Al
Khartoum.
Hii
ni mara ya pili kwa Azam FC kuingia fainali ya Kagame, mara ya kwanza
ikiwa ni 2012 ambapo ilifungwa na Yanga iliyokuwa ikifundishwa na Tom
Saintfiet ambaye sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Togo.

Post a Comment