Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa CUF Taifa
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof.Ibrahim Lipumba akiongea na wanahabari leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida kulia, Abdala Shabani pamoja na mdogo wake, Shabaani Miraji wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.

Akionyesha Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha rasimu ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amejiuzulu nafasi ya uenyekiti jijini Dar es Salaam leo.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Peacok jijini Dar, Lipumba amedai kuwa Ukawa wameshindwa kusimamia makubaliano hivyo atabaki kuwa mwanachama.Taarifa zaidi kuwajia hapo baadaye

Post a Comment