Licha ya kupata bwana mpya; Johari: Siachani na Ray!
Staa wa filamu Bongo, Blandina William Chagula ‘Johari’.
Brighton Masalu
SIKU chache baada ya
kupenyezwa kwa madai ya kupata bwana mpya, staa wa filamu Bongo,
Blandina William Chagula ‘Johari’ ameibuka na kuweka wazi kuwa kamwe
hafikirii wala hana mpango wa kuachana na msanii mwenzake, Vincent
Kigosi ‘Ray’ katika masuala ya kazi.
‘Akianika mwanya’ na Risasi Jumamosi
hivi karibuni ndani ya ofisi zake, Sinza-Mori jijini Dar, Johari alisema
hawezi kuruhusu mapenzi yatawale maisha yake na kusahau kazi.
“Siondoki RJ, kama kuna mtu anatarajia
nitoke hapa eti kisa mambo ya mapenzi, anajidanganya kabisa, sifikirii
kuachana na Ray kikazi, ni mtu muhimu sana, mapenzi hayawezi kutawala
maisha yangu, yeye atabaki na mpenzi wake na mimi nitaendelea na mpenzi
wangu,” alisema Johari.
Ray kwa sasa ameshaonesha upande na
kukiri kukolea kwenye penzi la mwigizaji Chuchu Hans na tayari
ameshajipambanua kuwa wana mipango endelevu maishani mwao.
Post a Comment