Flora amshtaki tena Mbasha akidai kumpa vitisho mara kwa mara!
Brighton Masalu
WAKATI
aliyekuwa mumewe akiwa na msala wa kubaka shemejiye mahakamani, mwimba
Injili Flora Mbasha amemshtaki tena mwandani wake huyo wa zamani,
Emmanuel Mbasha akidai kumpa vitisho mara kwa mara.
Emmanuel Mbasha.
Chanzo
kilicho karibu na Flora kilipenyeza habari kuwa mara kwa mara Mbasha
amekuwa akimtishia Flora ndipo mwanamuziki huyo alipoamua kumshtaki
polisi.
“Jamaa
(Mbasha) alikuwa akitumia watu kumtishatisha Flora sasa Flora akaamua
kwenda kumshtaki polisi Msimbazi maana ameona lolote linaweza kutokea
hivyo awe tayari ameshatoa mashtaka polisi,” kilisema chanzo hicho.
Mwanahabari
wetu alipomtafuta Flora na kumuuliza kama amemshtaki Mbasha, alikiri na
kubainisha kuwa alifanya hivyo kutokana na vitisho mbalimbali
alivyokuwa anavipata.
“Ni
kweli ilibidi niende pale Msimbazi Polisi, nikapewa jalada uchunguzi
MS/RB/7000/2014. Mbasha amekuwa akinitishiatishia sana, mara aniambie
nitahama nchi niende nikaishi kwa ndugu zangu Marekani,” alisema Flora.
Alipotafutwa Mbasha na kusomewa mashtaka yake, alisema Flora ni muongo na anatafuta kujitetea mbele ya jamii aonekane ni mwema.
“Hana
lolote huyo muongo tu, nilisikia hata mimi kuwa amenishtaki lakini
nafikiri hata polisi hawakulipa uzito jambo hilo na yaliisha
hivyohivyo,” alisema Mbasha.
Mbali
na tukio hilo, Mbasha anakabiliwa na kesi ya kumbaka shemeji yake kosa
analodaiwa kulitenda mwaka jana, jijini Dar. Juzi Alhamisi alifika
katika Mahakama ya Ilala na kutoa utetezi kisha kesi ikaahirishwa hadi
Agosti 14, mwaka huu.

Post a Comment