ad

ad

MARY MAWIGI AJIFUNGUA KIDUME KWA KISU

Msanii wa filamu za Kibongo, Mary Mawigi hivi karibuni amejifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Mico iliyopo Sinza jijini.
Akizungumza na Ijumaa, Mary alisema kuwa ana furaha sana ya kupata mtoto kwani ni kitendo alichokisubiri kwa muda mrefu na Mungu amemjaalia.
“Nina furaha sana kwa maana mtoto ni baraka ambayo nilikuwa nikiisubiri kwa hamu, nilitamani kumuonesha kila mtu amuone hadharani lakini baba yake hapendi watu watamuona hadi pale itakapobidi tu,” alisema Mary.
Powered by Blogger.