MANCHESTER UNITED KUMTOA JONNY EVANS NA PESA JUU ILI KUMNASA SEAMUS COLEMAN WA EVERTON
MANCHESTER UNITED inataka kumtumia Jonny Evans kama ndoano ya kumnasa staa wa Everton Seamus Coleman.
Bosi wa United Louis van Gaal anataka Seamus Coleman akamalize tatizo la beki ya kulia Old Trafford hasa baada ya kuwakosa Dani Alves na Nathaniel Clyne.
Everton imesisitiza kuwa Coleman hauzwi na kwamba United inapoteza bure muda wao kupeleka ofa kwaajili ya kupata saini ya beki huyo wa Ireland.
Lakini United bado inaamini kuwa biashara itafanyika na sasa inataka kutoa pesa na Jonny Evans juu ili kuongeza ushawishi kwa Everton.
Jonny Evans amebakiza miezi 12 ya mkataba wake na bado hajaona dalili ya kupewa dili jipya huku wenzake Chris Smalling, Phil Jones, Paddy McNair na Tyler Blackett wote wameshaanguka mkataba mpya.

Post a Comment