ad

ad

ESTER AZIDI KUTESWA NA TUMBO LA BIA

KUNENEPEANA! Kuvimbiana na kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo kunazidi kumpa wakati mgumu msanii ‘anayechungulia’ katika gemu la uigizaji, Ester Kiama kufuatia kusongwa na madai kuwa ‘amebugia kijusi’ (mjamzito) huku Kulwa Kikumba ‘Dude’ akidaiwa kuwa baba kijacho.
Msanii ‘anayechungulia’ katika gemu la uigizaji, Ester Kiama.
Akikutanisha ‘lips’ na paparazi wetu hivi karibuni, Ester alisema licha ya kuwaeleza watu kwamba ukubwa wa tumbo lake unatokana na utumiaji wa vinywaji vyenye ngano (kama bia) na uvivu wa kufanya mazoezi, lakini wao wamekuwa wakimkomalia kuwa ni mimba.
“Watu wengi wanasema nina mimba. Wengine wanakwenda mbele zaidi wakinipongeza kwa kumbebea mimba Dude. Yaani napata wakati mgumu,” alisema Ester.

No comments

Powered by Blogger.